HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 24, 2024

ELIMU YA MLIPA KODI ILIVYOMUOKOA MIKONONI MWA MATAPELI

 

MFANYABIASHARA Marik Ngutti wa Machimbo ya Matabi wilayani Chato Mkoa wa Geita ameeleza namna ambavyo ufuatiliaji wake wa elimu ya mlipa kodi ilivyomnasua kutoka kwenye mikono ya matapeli waliojifanya maofisa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Ngutti ametoa ushuhuda huo leo Aprili 23, 2024 alipotembelea banda la TRA katika maonesho ya Wakandarasi Geita Mjini kwenye viwanja vya EPZ ambapo amesema aliwapa elimu na wafanya biashara wenzake ambao pia walishindwa kutapeliwa baada ya kupata taarifa muhimu kuhusu maofisa wa TRA.

"Kuna watu walikuja kwenye maeneo yetu ya biashara pale Machimbo ya Matabi walijitambulisha kuwa ni maofisa wa TRA niliwajengea mashaka kwa kuwa niliona hawana utambulisho wa TRA na hawakuwa wanatoa lisiti kwa wenzetu waliotangulia kupita nikawaambia wafanyabiashara wenzangu kuwa hao sio maofisa wa TRA nikawapa namba ya TRA"

Amesema kwa kuwa tayari alishawapa elimu ya mlipa kodi walivyofika wale maofisa bandia wa TRA wale wafanyabiashara waliwahoji mambo muhimu yanayohusu TRA waliposhindwa kujibu wakaondoka zao na .

Ngutti amesema kuwa ufahamu juu ya masuala muhimu ya kodi na maofisa wa TRA ameyapata kutokana na jitihada zake za kufuatilia vipindi mbalimbali vya runinga na radio na kuwasisitiza wananchi wote kujielimisha katika masula muhimu ya kodi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad