WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) leo Machi 13, 2024 ameongoza Waombolezaji kuaga Mwili wa Marehemu Meja Jenerali Christopher Keraryo Gimonge (Mstaafu) katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo Jijini Dar Es salaam.
Akitoa salamu za rambirambi, Waziri Stergomena Tax aliwasilisha salaam za pole toka kwa Amri Jeshi Mkuu, Mhe Daktari Samia Suluhu Hassan,kwa kusema kuwa kuwa, Serikali pamoja na Jeshi limepoteza Kamanda na Kiongozi muhimu kwani wakati wa uhai wake, marehemu alilitumikia Jeshi katika nafasi mbalimbali kwa mafanikio makubwa ambapo ametoa wito wa kuiga yote mambo mema na uchapakazi aliounyesha marehemu Meja Jenerali Gimonge (Mstaafu)
Viongozi wengine waliohudhuria tukio hilo ni pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Wakuu wa Majeshi Wastaafu, Majenerali, Maafisa Wakuu, Maafisa Wadogo, Askari pamoja na waombolezaji, ambapo mwili wa Meja Jenerali Gimonge umesafirishwa leo kwenda Mkoani Mara kwa maziko.
No comments:
Post a Comment