HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 8, 2024

TRA YAMPATIA TUZO MWANAMKE MLIPAKODI WA KWANZA MWAKA 2023

Mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Zara Tours, Zainab Ansell, Leila Lankhan akipokea tuzo ya Mwanamke  mlipakodi namba moja mwaka 2023 kwa kumpatia tuzo na zawadi mbalimbali. Matukio hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya siku ya wananwake duniani inayofanyika Machi 8, kila Mwaka 

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
Katika kusherehekea siku ya Wanawake Duniani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imemtambua mwanamke mlipakodi namba moja mwaka 2023 kwa kumpatia tuzo na zawadi mbali mbali na kuwataka walipa kodi wengine kuiga mfano wake.

Zainab Addan Ansell ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Utalii ya Zara International Travel Agency kutoka Mkoa wa kodi Kilimanjaro ndiye amepokea tuzo hiyo.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake leo Machi 8, 2024, Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Hassan Mcha amesema tuzo hiyo ni hatua kubwa na yenye umuhimu katika kuleta mabadiliko na kuvutia mwanga kwa wanawake katika ulimwengu wa kodi.

"Tunakupongeza kwa juhudi zako katika kufanya kazi ya Utalii na mchango wako wa kipekee kuwa na ari kubwa ya kufanya tofauti. Endelea kung'aa na kuhamasisha wanawake wengine kufuata nyayo zako za mafanikio," amesema Mcha.

Kamishna Mcha pia ametoa wito kwa wanawake wa TRA kuendelea kuwa walinzi wa taswira nzuri ya Mamlaka hiyo kwa kuwa vinara wa uadilifu, weledi, uwajibikaji, na uaminifu katika kutekeleza majukumu ya utumishi wa umma ndani ya Mamlaka.

"Hii itaendelea kuweka taswira nzuri kwa wateja wetu tunaowahudumia na wakati huo huo tukijenga mahusiano mazuri na kuongeza ari ya ulipaji kodi wa hiari. Sote tunatambua kuwa wanawake ni jeshi kubwa hivyo mkisimama kidete katika hili mtaleta mabadiliko makubwa sana katika jamii yetu na kuiwezesha TRA kutimiza malengo yake ya ukusanyaji kodi kwa maendeleo ya taifa letu huku tukiunga mkono juhudi za Dk. Samia Suluhu Hassan," amesema Mcha.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mwakilishi wa Kampuni ya Utalii ya Zara International Travel Agency, Leila Lakhan ameishukuru TRA kwa kutambua mchango wake na ameahid kuendelea kulipa kodi zaidi na kwamba watahakikisha wanaendelea kulipa kodi kwa wakati ili hata mwakani waweze kupata tena tuzo hiyo.

Mapema, akitoa salamu kwa niaba ya wafanyakazi wanawake wa TRA, Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala, Renalda Lyimo amesema kuwa wanatambua juhudi zinazofanywa na wanawake wa Mamlaka hiyo katika kuhakikisha malengo ya Taasisi yanafikiwa kwa kuweza kukabiliana na majukumu mazito ya kukusanya Mapato ya Serikali kwa ufanisi wa hali ya juu ilihali wakiwa wana endelea kufanya majukumu yao ya kifamilia pia.


Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Hassan Mcha akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake leo Machi 8, 2024 jijini Dar es Salaam.













Maandamano yakiendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad