Na Mwandishi Wetu
WAKATI Wanawake wa Tanzania wakiungana nawenzao duniani kuadhimishia Siku ya Wanawake, Kampuni ya Puma imesema ni muhimu kundi hilo likaendelea kutazamwa kwa karibu.
Kampuni hiyo leo Machi 8, 2024 imekabidhi msaada wa vifaa tiba vikiwemo viti mwendo na vifaa vya kupima presha vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5 ambavyo vitatumika katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Fatma Abdallah amesema wanawake ni kundi linalopaswa kupewa uangalizi wa karibu si kwa kupendelewa lakini kutokana na umuhimu wao.
“Puma tumekuja kukabidhii vifaa tiba katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, tumejitahidi kukusanya vifaa tiba kadhaa vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5. Tunavyo vifaa tiba mbalimbali vikiwemo viti mwendo na mashine za kupima presha, tunaamini vitasaidia wodi ya wanawake. Tunafamu wodi ya akinamama ni eneo lenye changamoto nyingi na wagonjwa wengi.
“Hivyo inahitaji uangalizi tofauti, sio kwamba tunajipendelea sisi wanawake lakini wodi ya wanawake inahitaji uangalizi wa tofauti kidogo,” amesema Fatma ambaye kampuni yake imeendelea kuongeza idadi ya wafanyakazi wanawake.
Amefafanua kuwa, katika Kampuni ya Puma kuna wafanyakazi wanawake zaidi ya 48 na hatua kubwa imepigwa kaunzia mwaka 2023 alipokuwa akianza kuitumikia Puma ilikuwa na wafanyakazi wanawake asilimia 9, lakini sasa wamefika asilimia 16 huku akisisitiza kwamba wengi wameingizwa katika uongozi.
Hata hivyo, amesema wanaendelea kutengeneza mazingira kuwawezesha, kuwathaminisha na kuwaleta pamoja wanawaje walete maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
“Puma tutaendelea kusaidia sekta ya afya kama tulivyosema, tunaangalia sekta ya afya na sekta ya elimu,” amesema.
“Sisi tunaongoza katika soko la mafuta, lakini bado tunaendelea kukua, tunaimani maono yetu ni kuhakikisha tunafikia wananchi wengi ambao hawapati huduma ya mafuta kwa ukaribu.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi Matroni Eva Sambaya amesema wanashukuru kupatiwa vifaa hivyo na Puma imeonesha kuwathamini na kuwajali kwani ziko hospitali nyingi katika jiji la Dar es Salaam.
“Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani Puma mmeona haja ya kuja kwetu na kutushika mkono , vifaa hivi kwetu vitasaidia katika kutoa huduma katika wodi ya wanawake.”
Wakati huo huo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni(DMO) Dk.Lucas Ngamtwa amesema wanatoa shukrani za dhati kwa kampuni ya Puma kwa namna ambavyo wameguswa na kuamua kuwashika mkono katika hospitali hiyo.
“Hospitali yetu ni mpya bado tunachangamoto nyingi ikiwemo ya watalaam na vifaa tiba lakini kwa kutambua hilo Kampuni ya Puma mmeona mje mtushike mkono kwa kuhakikisha akina mama wanaokuja kupata huduma katika hospitali yetu wanakuwa salama na wanajifungua katika mazingira mazuri.”
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Fatma Abdallah (mwenye ushungi) akikabidhi msaada wa vifaa tiba vikiwemo viti mwendo na vifaa vya kupima presha vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5 ambavyo vitatumika katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Anayepokea ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni(DMO) Dk.Lucas Ngamtwa. Puma wamekabidhi msaada huo leo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Fatma Abdallah (mwenye ushungi) akikabidhi msaada wa vifaa tiba vikiwemo viti mwendo na vifaa vya kupima presha vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5 ambavyo vitatumika katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Anayepokea ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni(DMO) Dk.Lucas Ngamtwa. Puma wamekabidhi msaada huo leo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Fatma Abdallah (mwenye ushungi) na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Puma Davita Showe wakikabidhi msaada wa vifaa tiba vikiwemo viti mwendo na vifaa vya kupima presha vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5 ambavyo vitatumika katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Wanaopokea ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni(DMO) Dk.Lucas Ngamtwa, Kaimu Muuguzi Mfawidhi Matron Eva Sambaya na Kaimu Mganga Mfawidhi wa hopsitali ya Kibugumo Dk. James Mbapili.Puma wamekabidhi msaada huo leo Machi 8, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani
Watumishi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa hospitali ya Wilaya ya Kigamboni huku wakiwa wameshika vifaa tiba ambavyo Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania imekabidhi na kutumika katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Puma wamekabidhi msaada huo leo Machi 8, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani
Watumishi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa hospitali ya Kibugumo Kigamboni huku wakiwa wameshika vifaa tiba ambavyo Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania imekabidhi na kutumika katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Puma wamekabidhi msaada huo leo Machi 8, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Fatma Abdallah (mwenye ushungi) akiwa na baadhi ya watumishi wa kampuni hiyo wakipata picha ya pamoja na viongozi wa hospitali ya ya Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba vikiwemo viti mwendo na vifaa vya kupima presha vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5 ambavyo vitatumika katika wodi ya wanawake ya Hospitali hiyo. Puma wamekabidhi msaada huo leo Machi 8, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani
Watumishi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba vikiwemo viti mwendo na vifaa vya kupima presha vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5 ambavyo vitatumika katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Puma wamekabidhi msaada huo leo Machi 8, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani
Watumishi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba vikiwemo viti mwendo na vifaa vya kupima presha vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5 ambavyo vitatumika katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Puma wamekabidhi msaada huo leo Machi 8, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani.
Watumishi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba vikiwemo viti mwendo na vifaa vya kupima presha vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5 ambavyo vitatumika katika wodi ya wanawake ya Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Puma wamekabidhi msaada huo leo Machi 8, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
No comments:
Post a Comment