HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 27, 2024

TCAA YAFUTURISHA NA KUTOA MKONO WA EID KITUO CHA BUSARA

 


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeandaa halfa ya futari iliyojumuisha Watoto yatima Pamoja na wadau wa Usafiri wa Anga iliyofanyika Machi 27,2024 hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari amesema Mamlaka inathamini na kutambua wajibu wake katika jamii na kusisitiza huu ni muendelezo tu wa utamaduni wa kurejesha kwa jamii.

Sambamba na hafla hiyo Menejimenti ya TCAA imekabidhi mkono wa Eid kwa Watoto waliohudhuria hafla hiyo wanaolelewa katika kituo cha Busara kilichopo Banana jijini Dar es Salaam.

Huu ni muendelezo wa Mamlaka kugusa jamii ambapo Machi 24,2024 TCAA ilitoa mkono wa Pasaka kwa kituo cha kulea Watoto yatima na wenye uhitaji cha ZILI House of Child Care kilichopo Kipawa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akipata futari Pamoja na Watoto wanaolelewa katika kituo cha Busara kilichopo Banana jijini Dar es Salaam wakati wa futari iliyoandaliwa na TCAA.
Sheikh Issa Othman akitoa neno wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akiongoza menejimenti ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga kukabidhi mkono wa Siku Kuu ya Eid kwa Watoto wanaolelewa katika kituo cha Busara kilichopo Banana jijini Dar es Salaam wakati wa futari iliyoandaliwa na TCAA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akifuturu na  Watoto wanaolelewa katika kituo cha Busara kilichopo Banana jijini Dar es Salaam wakati wa futari iliyoandaliwa na TCAA.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na   Watoto wanaolelewa katika kituo cha Busara kilichopo Banana  wakiwa kwenye hafla ya  futari iliyoandaliwa na TCAA.
Picha za pamoja 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad