HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 12, 2024

CATC YATEMBELEWA NA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA SHABAN ROBERT

 Jumla ya wanafunzi 32 wa shule ya sekondari ya Shaban Robert wametembelea Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) katika ziara ya kimasomo na kupata fursa ya kujifunza na kujionea mambo mbalimbali.


Wanafunzi hao wa kidato cha nne na cha tano wanaochukuwa masomo ya sayansi walipata elimu ya jumla kuhusu CATC na shughuli zake kutoka kwa Mkuu wa Mafunzo Didacus Mweya.  

Wanafunzi hao walioambatana na mwalimu wao Boniface Mkali walipata fursa pia ya kutembelea mtambo wa kufundishia waongoza Ndege na kujionea namna unavyofanya kazi na kupata fursa ya kumuuliza maswali msimamizi wa mtambo huo Neema Senyagwa.

CATC moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.
Msimamizi wa Mtambo wa kufundishia waongoza Ndege Neema Senyagwa akitoa maelezo namna mtambo huo unavyofanya kazi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Shaban Robert waliotembelea  Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) katika ziara ya kimasomo na kupata fursa ya kujifunza na kujionea mambo mbalimbali chuoni hapo.
 Mkuu wa Mafunzo kutoka CATC Didacus Mweya akitoa elimu kwa kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Tano wa shule ya sekondari ya Shaban Robert kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho wakati wa ziara ya kimasomo na kupata fursa ya kujifunza na kujionea mambo mbalimbali chuoni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne na Tano wa shule ya sekondari ya Shaban Robert wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na Mkuu wa Mafunzo kutoka CATC Didacus Mweya wakati wa ziara ya kimasomo na kupata fursa ya kujifunza na kujionea mambo mbalimbali chuoni hapo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne na Tano wa shule ya sekondari ya Shaban Robert  waliofika Chuoni hapo kwa ziara ya kimasomo na kupata fursa ya kujifunza na kujionea mambo mbalimbali chuoni hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad