HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 8, 2024

Y9 Inc yazindua simu benki ya kwanza duniani!

Y9 Inc iliyosajiliwa USA, inayoendesha biashara Tanzania kama Y9 Microfinance ni kampuni yenye malengo ya kupunguza pengo la watu wasiokuwa na vigezo vya kukopeshwa katika masoko yanayoibuka kwa njia bora na yenye manufaa. 

Kutokana na malengo hayo wamezindua simu ya kwanza duniani inayojuisha huduma za simu na za mikopo midogo ili kurahisisha shughuli za biashara.

Ashok Kavinattamai, Mkurugenzi Mtendaji wa Y9 Microfinance Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Y9 Inc nchini, alielezea furaha yake kuhusu uzinduzi wa simu hiyo. 

Akisema,  “malengo yetu yanaelekezwa kwenye kuwawezesha Watanzania katika ushirikishwaji wa kidijitali na kifedha. Simu hii inayoitwa TZ1 ni ya kisasa kiteknolojia na ina kasi ya 4G. 

Y9 Microfinance pia hutoa huduma ya mikopo ya Simu, tunaendelea kupiga hatua kuelekea kufanya teknolojia  ya kisasa kuwa ya uhalisia kwa kufikisha huduma hii kwa watu wengi zaidi nchini. Lengo letu ni kupunguza pengo, kuhakikisha kwamba kila mtu, bila kujali hali yake ya kiuchumi, anaweza kunufaika na faida za kimtandao na kurahisisha ufikiaji wa huduma za kifedha."

Kila Mtanzania sasa anaweza kumiliki simu ya kisasa yenye kasi ya 4G, iliyotengenezwa na teknolojia ya kisasa kama vile mfumo wa malipo ya "Tap pay" ambao hii simu itawezeshwa nayo, pia ikiwa na programu zote maarufu za mitandao ambazo zinaifanya TZ1 kuwa juu kulinganishwa na simu nyingine za rika lake; kuthibitisha ahadi ya Y9 Microfinance ya kutoa huduma za mikopo ya simu kwa watu wote.

 Zaidi ya hayo, Y9 Microfinance inaingia sokoni, kuvunja vizuizi na kuwezesha ufikiaji wa kidijitali wa 4G na huduma za kifedha kwa watu wote.

Huduma za mikopo wa Simu huwa ni nafuu kwa watu ambao huona gharama ya kununua simu janja  ni kikwazo. Kwa kuongeza TZ 1 ni ya kisasa na yenye kasi ya 4G,  na ni  bei nafuu. 

Y9 Microfinance pia hutoa huduma kama vile mikopo ya pesa taslimu, mikopo ya fedha za matumizi na mikopo ya mshahara kidigitali, kupitia simu janja.  Y9 Microfinance, inalenga kuwezesha idadi kubwa ya watu, kutumia na kunufaika na kasi ya mtandao, huduma za kidijitali kwa ukuaji wa kibinafsi na kifedha. 

Huduma ya mkopo wa Simu ya Y9 Microfinance inalenga kurahisisha malengo ya kukuza matumizi ya kidijitali kote Tanzania. Taasisi inatazamia mustakabali ambapo kila mtu, bila kujali hadhi yake ya kiuchumi, aweze kuwa na zana na fursa ya kushiriki kwa maana katika uchumi wa kidijitali.

Bw. Kavinattamai alisisitiza mabadiliko haya, akiongeza, "Uzoefu wetu wa kutoa simu za mkononi zenye kasi ya 4G ulionyesha uhitaji ya teknolojia hii, tulitambua hitaji la kufikia hadhira kubwa zaidi. Huduma ya mkopo wa Simu ni jibu letu kwa hili, kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma katika mapinduzi ya kidijitali."

Y9 Inc imejitolea kupanua biashara zake za kidijitali katika nchi kadhaa za Afrika na zaidi. Na tayari wapo kwenye mazungumzo na taasisi nyingine kuboresha ushirikiano wa bidhaa za Y9 katika masoko  ili kuharakisha ukuaji na kuondoa vizuizi vya kidijitali na kifedha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad