HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 24, 2024

TIC na Benki ya CRDB zaingia makubaliano ya ushirikiano

*Ni katika kutoa huduma kwa wawekezaji kwa mifumo ya kusomana

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimeingia makubaliano ya ushirikiano na Benki ya CRDB ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi kwa wawekezaji.

Akizungumza mara baada ya kusaini hati za Makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa TIC Gilead Teri amesema kuwa ushirikiano ni kutumia ujuzi baina ya taasisi mbili katika kuwahudumia wateja kwa ufanisi.

Amesema kuwa CRDB ina wateja wengi wa ndani na nje hivyo itakuwa ni rahisi kutoa huduma kwa mwekezaji kwa mfumo mmoja wa Tehama ambapo haitawachukua muda mrefu kwa mwekezaji.

Teri amesema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Desemba miradi 61 imesajiliwa ambapo ni watanzania ambapo imeonyesha kuwa na mwitikio mkubwa hata kwa wawekezaji wa ndani.

Amesema kuwa kuongezeka kwa wawekezaji kumetokana na jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kufungua mipaka.

Aidha amesema kadiri wawekezaji wanavyowekezaji wa ndani na nje wanavyowekeza wanaongeza ajira katika sekta binafsi.

Teri amesema kuwa timu TIC imejipanga katika kutoa huduma bora kwa viwango vya kimataifa suala zima la uwekezaji nchini kwa kwenda na dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wawekezaji wanapata huduma katika ofisi hizo bila kuwa changamoto yeyote.

Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB Boma Ruballa amesema kuwa watashirikiana na TIC katika kuhudumia wawekezaji ambao ni wateja wa CRDB kwa kutumia mfumo wa Tehama unaosomana .

Amesma kuwa CRDB kutokana na kuwa na wateja hadi nje ya nchi itakuwa rahisi katika utoaji wa huduma kwa wale watakuwa wawekezaji .
 

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri na  Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB Boma Ruballa wakisaini makubaliano ya ushirikiano katika  kwenye kutoa huduma kwa wateja kwenye uwekezaji ,jijini Dar es Salaam.
 

Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB Boma Ruballa akizungumza kuhusiaana kushikiana na TIC katika  kwenye kutoa huduma kwa wateja kwenye uwekezaji ,jijini Dar es Salaam.
 

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri na  Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB Boma Ruballa wakiwa na hati ya  makubaliano ya ushirikiano katika  kwenye kutoa huduma kwa wateja kwenye uwekezaji ,jijini Dar es Salaam.
 

Picha ya pamoja kati wafanyakazi wa TIC na Mkurugenzi Mkuu wa TIC Gilead Teri mara baada ya kusaini hati za makubaliano na Benki ya CRDB,jijini  Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad