HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 24, 2024

SHEIKH MKUU WA TANZANIA AONGOZA DUA KULIOMBEA TAIFA, KILELE CHAKE JUMAMOSI

 

 VIONGOZI ya dini ya Kiislamu pamoja na waumini wa dini hiyo na wananchi kwa ujumla leo wameingia katika siku ya pili ya kuendelea na dua maalum ya kuliombea Taifa pamoja na viongozi wote.


Katka dua ya leo Ijumaa Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Bin Zubeir akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini pamoja na Mjumbe wa Halmashauri  ya BAKWATA Ahmed Misanga ni miongoni walioshiriki katika dua hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba imeelezwa kuwa leo Ijumaa ni siku ya pili ya mwendelezo wa wa dua hiyo kubwa iliyotangazwa kufanya na Mufti wa Tanzania kwa mfululizo wa siku tatu na kilele cha dua hiyo ni Februari  24 mwaka huu ambayo itakuwa Jumamosi.

Kilele cha dua hiyo  katika viwanja vya Msikiti wa Mfalme Mohammed VI BAKWATA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam huku ikisisitizwa katika siku hiyo dua itaanza saa mbili asubuhi hadi saa 10 alasiri.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad