HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 15, 2024

MELI TANO ZA WATALII ZATIA NANGA BANDARI YA KILWA MWEZI FEBRUARI

Mwaka 2024 umeanza kwa rekodi ya ufanisi wa hali ya juu katika kupokea Watalii wanaotumia Bandari ya Kilwa ambapo kwa Mwezi Februari pekee, Meli tano za Watalii zimetia nanga Bandarini hapo na kuhudumiwa.

Bandari ya Kilwa iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, imeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa Watalii kutoka Mataifa mbalimbali ambao wanaendelea kuwasili Nchini kujionea vituo vya Utalii.

Meli ya Watalii ya BOUGAINVILLE ambayo ni Meli ya tano kutia nanga Bandarini hapo, imewasili ikiwa na Watalii 133.

Tangu kuanza kuwasili kwa Meli hizo, jumla ya Watalii 593 Wametembelea Vivutio vya Utalii kwa mafanikio na kusifu huduma za Meli zinazotolewa na Wataalamu Wazawa wa TPA ambao wameonesha Weledi na umahiri mkubwa katika majukumu yao ya kuhudumia Meli hizo za Watalii.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad