HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 13, 2024

BALOZI WA TANZANIA NCHINI MSUMBIJI AKUTANA NA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA EDUARDO MONDLANE

Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, amekutana na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Eduardo Mondlane Cha Msumbiji ulioongozwa na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Doutor Manuel Guilherme Junior, leo tarehe 13 Februari, 2024.

Katika mazungumzo yao, pande mbili zilikubaliana kuimarisha uhusiano na ushirikiano (kati ya Tanzania na Msumbiji) katika sekta ya Elimu, hususan kuanzishwa Darasa la Kiswahili Chuoni hapo na Darasa la Kireno katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania, Maputo.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad