HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 9, 2024

UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO MKOANI TABORA

 

WATAALAM wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE iliyopo Mkoani Tabora watatoa huduma za tiba mkoba zinazojulikana kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Tabora na mikoa ya jirani.

Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia tarehe 15/01/2024 hadi tarehe 19/01/2024 saa mbili kamili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni katika Viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE.

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Tunaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0754687666 Dkt. Mark Waziri, 0714292222 Dkt. Ally Remtullah na 0737763298 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad