HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 4, 2023

Waajiri Wakumbushwa kuweka Mazingira wezeshi na Jumuishi kwa watu wenye ulemavu

 WAAJIRI Wakumbushwa kuweka Mazingira wezeshi na Jumuishi kwa watu wenye ulemavu ili kuwepo kwa usawa na usalama mahala pa kazi na kuwavutia wawekezaji.


Akizungumza jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako wakati wa kugawa tuzo ya kutambua mwajiri bora wa mwaka 2023, amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na Chama cha Waajiri (ATE) Katika kupigania maslahi ya waajiri wote nchini na kutengeneza mazingira wezeshi na Jumuishi kwa waajiri.

Ndalichako ameongeza kuwa Waziri Mkuu anawapongeza wadau mbalimbali ikiwemo TUCTA kwa kufanya kazi pamoja ili kuongeza tija kwenye serikali yetu. Kipekee nampongeza mshauri elekezi aliyekamilisha mchakato wote wa kuwapata washindani waliopata tuzo siku ya leo.

"Nawapongeza sana Washiriki wote na kama wahenga walisema asiyekubali kushindwa sio mshindani, na mchakato ulionesha Ushindani wa hali ya Juu na ninawapongeza sana ATE kwa kuratibisha mchakato huu." Amesema Ndalichako

Aidha amesisitiza kuwa tuzo hizo zitawasukuma zaidi hata wale ambao hawaja pokea tuzo ili kipindi kijacho waweze kushiriki kushindania na hata wale ambao wameibuka washindi waendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuonesha walistahili kupokea tuzo hizo.

"Nawapongeza Sana ndugu waajiri kwa kufanya kazi na Serikali ili kuhakikisha sehemu zote za kazi ziko salama na kuhakikisha Usalama mahali pa kazi halina budi kutiliwa mkazo na kupewa kipaumbele kwanza."

Moja ya vipengele vilivyozingatiwa ni vile vinayotambua mahitaji ya watu wanaoishi na Ulemavu mahali pa kazi. Hivyo waajiri wote wanapaswa kuwajumuisha katika waajiriwa 20 basi 3% wawe watu wanaoishi na Ulemavu.

Kwa Uapnde wa Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri (ATE) Suzanne Ndomba amesema tuzo ya Mwajiri Bora kwa Mwaka huu ina na vipengele 14 ambavyo vimejikita katika maeneo mbalimbali ambayo yamelenga kuongeza chachu kwa waajiri ili kuongeza tija na ushindani.

"Naomba pia nitumie fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini ni ombi letu kwamba juhudi hizi ziendelee kwa kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini."

Aidha ameiomba Serikali kupitia Sheria zao ili ziandane na wakati, kuendelea kupunguza tozo mbalimbali ambazo zinaongeza gharama ya kufanya biashara ili kuendelea kuwavutia wawekezaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu.

"ATE kama sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Ushauri la Taifa kwa Watu Wenye Ulemavu nchini, tumeendelea pia kutambua umuhimu wa kujenga mazingira yanayojali mchango wa watu wote hususani wenye ulemavu."

Pia ndomba ameeleza kuwa tuzo hizo, zimeendelea kutambua mwajiri anayezingatia umuhimu wa kuwa na mazingira wezeshi kwa Wenye Ulemavu ili kuhamasisha waajiri kuweka mazingira yenye staha na rafiki yanayowawezesha watu wenye ulemavu kufanya kazi na kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu.

Aidha Kampuni mbalimbali zimeibuka ikiwemo Mshindi katika Kipengele cha Usawa wa Kijinsia na usawa katika Maeneo ya kazi imeibuka mshindi Benki ya NMB,wakati Mshindi wa kipengele cha Makampuni yanayokabiliana na majanga yanayotokea imeibukq ushindi kampuni ya Barrick gold mine, Mshindi wa Kipengele cha Mabadiliko ya tabia ya nchi imeibuka WWF, Mshindi katika Kipengele uwajibikaji katika Mwenendo biashara na utendaji unaokidhi imeibuka na ushindi Benki ya CRDB, Mshindi wa Kipengele cha Maudhui ya Ndani imeibuka ushindi benki ya Stanbic.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa Kugawa tuzo ya kutambua mwajiri bora wa mwaka 2023 tuzo zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri  (ATE) Mlimani City Jijini Dar es Salaam akisisitiza zaidi Waajiri kueka mazingira wezeshi na Jumuishi kwa watu wenye Ulemavu nchini
Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri (ATE) Suzanne Ndomba akiongea machache wakati akikaribisha wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya ugawaji tuzo za mwajiri bora wa mwaka 2023 zilizofanyika Leo Disemba 04,2023 Mlimani City Jijini Dar es Salaam
Picha ya tuzo za vipengele mbalimbali zilizoshindaniwa kwa Makampuni zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini (ATE) zilizofanyika leo Disemba 04,2023 Mlimani City Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad