HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 15, 2023

Mashirika 16 yaunganishwa pamoja na Mashirika Manne yafutwa

 Na Chalila Kibuda,Michuzi TV 


Mashirika 16 ya Umma yameunganishwa kwa kuwa taasisi moja huku mashirika Manne yakifutwa ni kuongeza tija katika mashirika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof Kitila Mkumbo amesema mageuzi hayo yataendelea ili kuweza kuleta maendeleao kutokana na kazi wanazozifanya.

“kuimarisha mashirika ya umma ili yaweze kuendelea kutoa mchango katika maendeleo ya Taifa” 

Amesema Katika kutekeleza hili Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia hotuba yake ya Bungeni ya tarehe 22 Aprili 2022 alielekeza, pamoja na mambo mengine, “...kufanya mapitio na uchambuzi wa kina kwenye uendeshaji wa Mashirika ya Umma, tukiwa na lengo la kuyafanya yaweze kujiendesha kwa faida” amesema Kitila

Profesa Kitila amesema katika muktadha SerikaliiliundaTimu ya Wataalam kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa kina kuhusu utendaji wa mashirika ya umma kwa lengo la kubainisha changamoto za kiutendaji na kupendekeza hatua za kuchukua katika kuongeza tija ya maendeleo ya nchi.

Aidha katika uchambuzi wa utendaji wa mashirika ya umma, Serikali inaongozwa na misingi mikubwa minne. Mosi, kuendelea kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli za uwekezaji na biashara. Katika kutekeleza hili, sekta ya umma itajielekeza katika maeneo yasiyovutia uwekezaji wa sekta binafsi. Mashirika ya umma yatahimizwa kuwekeza katika maeneo ya kimkakati kulingana na majukumu yao. 

Waziri Profesa Mkumbo Serikali itaelekeza rasilimali nyingi kwenye miradi mikubwa yenye matokeo ya muda mrefu, hususani, ile isiyovutia sekta binafsi kuwekeza. Pili, Serikali kupunguza mzigo wa kuendesha mashirika ya umma yanayohitaji ruzuku.

Mashirika na Taasisi za umma zilizounganishwa 

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini ( RITA) yanaunganishwa na kuunda taasisi moja inatayohusika na utambuzi wa matukio muhimu maishani. 

Wakati huo Benki ya Kilimo Tanzania (TADB) na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) zinaunganishwa ili kuwa na taasisi moja itakayohusika na mikopo na ugharamiaji wa maendeleo ya kilimo nchini.

Bodi ya Chai inaunganishwa na Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania (Tanzania (TSHDA) zinaunganishwa ili kuwa na bodi moja Bodi ya chai.

Bodi ya. Nyama inaunganishwa na Bodi ya Maziwa zinaunganishwa ilikuunda taasisi moja ya kuendeleza na kusimamia mazao ya mifugo yakiwemo ya nyama na maziwa

Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CARMARTEC), Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) zinaunganishwa ili kuunda taasisi moja.

Kituo cha UwekezajiTanzania(TIC) kinaunganishwa na Mamlaka ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) ili kuunda taasisi moja itakayoratibu uwekezaji wa sekta binafsi wa ndani na kutoka nje ya nchi.

Taasisi ya Utafiti wa Chai Tanzania (TRIT) Taasisi ya Utafiti wa Tumbaku Tanzania (TORITA) na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa ((TACRI) zinaunganishwa na kuwa sehemu ya muundo wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Mashirika na Taasisi za Umma zilizofutwa na kuvunjwa Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi (TPFCS), Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Shirika la Elimu Kibaha (KEC) linavunjwa na kuunda Shule ya Sekondari Kibaha ama kwa jina ambalo Mamlaka husika zitaamua na Chuo Cha Ufundi.

Kwa uamuzi huo hospitali ya Tumbi Kibaha haitakuwa tena sehemu ya Shirika la Elimu Kibaha bali hospitali ya Mkoa wa Pwani na Msajili wa Hazina ameshaelekezwa kukamilisha taratibu husika za makabidhiano na Wizara ya Afya.

Bodi ya Pareto inafutwa na shughuli zake zitahamishiwa katika Mamlaka ya Usimamizi wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (-COPRA)

Amesema Katika mchakato huo mambo matatu yafuatayoyatazingatiwa ambapo hakuna mtumishi atakayepoteza ajira yake. Maslahi yote watumishi ya umma katika mashirika na taasisi husika yatalindwa na kuzingatiwa kikamilifu kwa kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma.

Amesema kuwa katika mashirika na taasisi nyingi za umma na serikali kwa ujumla kuna upungufu mkubwa wa watumishi wa umma.

Amesema watumishi wote ambao mashirika na taasisi zao zinaguswa na zoezi hilo watapangiwa kazi zingine katika utumishi wa umma na maslahi yao yatazingatiwa ipasavyo.

Profesa Mkumbo amesema Mchakato wa kufuta na/au kuunganisha mashirika na taasisi za umma utazingatia sheria ambazo zimeanzisha taasisi hizo ni kwa sababu na uamuzi ninaoutangaza hapa tayari ulishawasilishwa kwa Mawaziri husika ambao ndio wenye nyezo husika hatua zao stahiki.

Mawaziri husika wameshaelekezwa kuhakikisha kuwa mchakato wa kufuta na au kuunganisha mashirika na taasisi za umma zilizotangazwa uwe umekamilika ndani ya mwaka huu wa fedha pamoja na mageuzi katika utendaji na uendeshaji wa Mashirika ya Umma ni zoezi endelevu. 

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya kupima na kutathimini utendaji wa mashirika na taasisi za umma kwa lengo la kuongeza tija katika maendeleo ya nchi.Waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza kuhusiana na mageuzi ya mashirika ya Umma kuunganishwa na mengine kufutwa ,bikini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad