"MDH ilishinda kama Mshindi wa kwanza wa Taarifa ya Fedha iliyowasilishwa Bora kwa mwaka wa 2022 katika kitengo cha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayoripoti kwa kutumia IPSAS. Tuzo hii ilitolewa na Bodi ya Kitaifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwenye Kongamano la Mwaka la 2023 la NBAA. Kwa miaka miwili mfululizo (2020 na 2021) MDH imekuwa Mshindi wa Pili kwenye kitengo kimoja. “Tuzo hii inaonyesha uaminifu, uwajibikaji na uwazi kwa serikali, washirika, wakiwemo wafadhili wetu na watu tunaowahudumia,” Alisema CPA. Damasco Peter, Mkurugenzi wa Fedha MDH.



No comments:
Post a Comment