HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 16, 2023

“TANZANIA NI SEHEMU SALAMA KWA BIASHARA NA UWEKEZAJI” WAZIRI MAKAMBA

  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), amezihakikishia sekta binafsi na za umma nchini Uholanzi kuwa Tanzania ni sehemu salama ya biashara na kuwekeza.


Hayo yameelezwa wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uholanzi lililofanyika jijini The Hague, Uholanzi tarehe 14 Novemba 2023.

Kongamano hilo lililotanguliwa na mkutano wa ndani kati ya sekta za umma na binafsi za nchi hizo, ambapo zilitumia fursa hiyo kujadili kwa kina fursa zilizopo Tanzania pamoja na taratibu nyingine zinazotakiwa kufuatwa na wawekezaji na wafanyabiashara kutoka mataifa mengine.

Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu isemayo “Ushirikiano sawa kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu” liliandaliwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini The Hague, Uholanzi kwa kushirikiana na Baraza la Biashara kati ya Uholanzi na Afrika (NABC).

Akifungua kongamano hilo Waziri Makamba pia alieleza kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka azma ya kutekeleza kwa vitendo dira ya Serikali ya kufanikisha ushindani na uanzishaji wa viwanda kwa maendeleo ya Taifa.


Kongamano likiendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad