HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 14, 2023

ROTARY KUTOA HUDUMA YA UPIMAJI AFYA BURE


· Kufanyika katika shule ya msingi Bunju Novemba 18, 2023

· Wakazi wa Dar watakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao

· Maandalizi yote yamekamilika

Mamia ya wakazi wa Bunju na maeneo ya Jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi Novemba 18 2023 katika viwanja vya shule ya msingi bunju kupima afya zao katika kambi maalum ya afya itakayoendeshwa na Rotary Tanzania.

Rotary ikishirikiana na wadau mbalimbali wa afya na wafadhili, wataendesha huduma hiyo siku nzima ya Jumamosi Novemba 18, ili kuwawezesha wakazi wengi wa Bunju, maeneo ya Jirani na Dar es Salaam kwa ujumla kupata mud awa Kwenda kupima afya zao na kupata ushauri wa kitaalamu bure bila malipo yoyote.

Jumla ya wakazi 5000 kutoka Bunju na maeneo ya jirani watapata huduma za afya na elimu bila malipo wakati wa tukio la siku ya Afya ya Rotary inayofanywa kwa ushirikiano na Vilabu vya Rotaract vya Kairuki, Muhimbili, KIUT, Alpha, na Kwanza. Inakadiriwa kuwa kuna wanafunzi 3500 na watu wazima 1500 watakaoshiriki, na kila mmoja wao atapata huduma muhimu kama vile vipimo, na elimu ya afya na kinga, uchunguzi wa macho, uchunguzi wa saratani mbali mbali, ukaguzi wa meno, elimu ya hedhi salama, na fursa ya kupata chanjo, dawa na rufaa za wataalamu kama itahitajika.

Kwa moyo wa kujitolea, madaktari takribani 100 - wakiwemo madaktari wa kawaida 50 na wataalamu wengine 50 wa meno, macho, ngozi, watoto, na huduma nyingine - wameahidi kutoa msaada wao kwa kutoa huduma hizi muhimu. Timu kubwa ya wahudumu takribani 500 inaunga mkono juhudi hizi, na ushirikiano huu unasisitiza umuhimu wa upendo na umoja katika kukabiliana na mahitaji ya afya ya jamii.

Mratibu wa zoezi hili kitaifa ambaye pia na Gavana mstaafu wa Rotary kanda ya Tanzania na Uganda Harish Bhatt amesema Zoezi ni kutekeleza moja ya azma za Rotary hususan katika kusaidia jamii kwenye Nyanja ya Afya. “Afya ni moja ya maeneo ambapo Rotary imewekeza sana na inashirikiana na wafadhili, serikali, taasisi na wanajamii katika kuhakikisha kuwa huduma za afya zinapatikana kwa wanajamii bila ubaguzi”

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Mehreen Khatri amesema maandalizi yote yamekamilika na amewashauri wakazi wa Dar es Salaam kutumia fursa hii adhimu kuja na kupima afya zao Pamoja na kupata ushauri na elimu ya afya. “tunashukuru maandalizi yote yamekamilika. Hii ni kutokana na ushiriki mkuwa wa wanachama wa Rotary Tanzania Pamoja wafadhili wetu. Tunaamini watu wengi watajitokeza kupima afya zao siku hiyo” alisema Mehreen.

Diamond Carvalho, Mwenyekiti wa Rotary Tanzania, alieleza, "Rotary Tanzania, kwa kushirikiana hasa na Klabu ya Rotary ya Oysterbay, imekuwa ikiandaa kambi za matibabu kwa ushirikiano na Klabu ya Rotaract ya Kairiuki tangu mwaka 2012, lengo likiwa kutoa huduma za afya msingi kwa jamii ya Dar es Salaam. Kampeni ya afya ya leo inaadhimisha hatua muhimu sana, ikiwa imeongezeka mara tatu ukubwa wa kambi za matibabu zilizofanywa hapo awali na klabu yetu. 

Tunapenda kuwashukuru sana Vilabu vya Rotary na Rotaract washirika wetu, vilevile washirika muhimu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Awamu ya Sita Ikiongozwa na Raisi Doctor Mama Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Afya, Bill & Melinda Gates Foundation, Guaranty Trust Bank, Pepsi, SGA Security, Jollie Pads, Agha Khan Health Service, Manufaa Media, Bakhressa Group ,Chemi Cotex, Hitech Sai Hospitals, Afya Intelligence na Management and Development for Health (MDH)."Mwenyekiti wa Rotary Tanzania,Diamond Carvalho,wakati akizungumza na waandishi wa habari masaki jijini Dar es Salaam alipokuwa akielezea kuhusu maandalizi ya kambi hiyo ya siku moja itakayofanyika Bunju jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi Novemba 18 2023.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad