HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 14, 2023

MEYA DSM AHIMIZA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA KABLA YA KUUGUA

 Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akipata maelezo kutoka kwa Meneja  Uhusiano wa NHIF Anjela Mziray wakati Meya huyo alipotembelea  banda la NHIF  katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasioambukiza yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akisaini kitabu cha wageni katika banda la NHIF wakati alipotembelea banda hilo katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasioambukiza yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akipata akisoma machapisho mbalimbali kwenye  banda la NHIF katika Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasioambukiza yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Na mwandishi wetu 
Wananchi wamehimizwa kujiunga na bima ya afya kabla ya kuugua uli wawe na uhakika wa matibabu pindi wanapopata janga la kuugua.

Hayo yamesemwa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary S. Kambilamoto alipotembelea banda la NHIF  katika Maadhimisho ya  Wiki ya Magonjwa Yasiyoambukiza inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Akizungumzia hili aliwataka wananchi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi wiki hii kuja kupima afya zao na kupata elimu ya kujiepusha na magonjwa haya na umuhimu wa kuwa na bima ya afya.

"Magonjwa yasioambukiza yanaepukika endapo kila mtu atazingatia kuishi mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi na kula lishe bora. Aidha, kila mtu azingatue kuwa na bima ya afya ili endapo atapata ugonjwa aweze kutibiwa bila kikwazo", amesema Mhe.  Kambilamoto.

Naye Meneja Uhusiano wa NHIF Bi. Anjela Mziray akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na Mfuko katika maadhimisho hayo yaliyoanza tarehe 11 na kupangwa kuisha  18 Novemba, 2023 amesema gharama za matibabu kwa magonjwa yasiyoambukiza ni kubwa hivyo elimu ni muhimu kuendelea kutolewa. 

Akitoa takwimu za matibabu ya magonjwa haya amesema kwa wastani gharama za matibabu kwa mgonjwa wa saratani kwa mwaka ni Sh. 69.9 milioni na kwa matibabu ya figo ni Sh. 35.8 milioni kwa mwaka. Aidha, amesema tathmini za jumla ya  malipo ya NHIF kwa matibabu ya saratani yameongezeka kutoka Sh. 12.2 bilioni kwa mwaka 2016/17 hadi Sh. 32.4 mwaka 2021/22. Kwa matibabu ya figo, jumla ya malipo hayo yameongezeka kutoka Sh. 11.4 bilioni mwaka 2016/17 hadi Sh. 35.4 bilioni kwa mwaka 2021/22.

" Takwimu hizi zinaonesha changamoto ya ugharamiaji wa magonjwa haya ni kubwa na elimu ya kujiepusha ni msingi pamoja na watu kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua" amesema Bi. Mziray

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad