HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 23, 2023

HUDEFO KUPITIA EPR YAWANOA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MADHARA YA TAKA ZA PLASTIKI

 

Na Mwandishi Wetu Bagamoyo

TAASISI ya Human Dignity and Environmental Care Foundation (HUDEFO) imeamua kuandaa semina maalum ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini kuelewa kuhusu madhara ya plastiki na jinsi gani wanaweza kushiriki katika kuiwezesha jamii kuepukana na madhara yatokanayo na  plastiki.

Semina hiyo ya kuwajengea uwezo waandishi hao ambao wanatoka mikoa mbalimbali inafanyika kupitia Mradi wa Extendend Produver Responsibility(EPR).Mradi huo unatekelezwa na HUDEFO ambaye ameshirikiana na Chuo Kikuu Dar es Salaam, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini (NEMC), serikali za mitaa, watafiti mbalimbali na sekta binafsi.

Akizungumza  wakati wa semina hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa HUDEFO Sarah Pima, Mshauri Mwelekezi Aman Mhinda amesisitiza lengo la semina hiyo ni kuwajengea uelewa kuhusu madhara yanayotokana na uwepo wa matumizi ya taka plastiki.

"Pia kupitia semina hii  tunaihamasisha Serikali kuendelea kuwa na mikakati ya kisheria na miongozo ya kiutendaji kwa wazalishaji ikiwa pamoja na ukusanyaji na uondoaji wa taka za  plastiki baada ya kutumika, "amesema Mhinda.

Akielezea zaidi kuhusu taka za plastiki, amesema pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa plastiki duniani pamoja na matumizi yake lakini ni asilimia  14 tu ya  plastiki ndizo zinarejeshwa kwa ajili ya recycling huku akifafanua takwimu zinaonesha kwa mwaka metric tani milioni 350,000,000 za plastiki huingia katika mfumo wa  matumizi.

Aidha amesema kuwa uwepo wa plastiki hizo umesababisha maeneo mengi kuwa na taka za plastiki na miongoni mwa maeneo hayo ni kwenye vyanzo vya maji kama baharini,  ziwani na mito kutokana na kusafirishwa kwa njia mbalimbali na plastiki hizo zinaathari nyingi zikiwemo za kiafya na kimazingira.

Amesema kuwa taka za plastiki ziko nyingi kuliko zinazoonekana na utafiti unaonesha kwamba ifikapo mwaka 2050 plastiki kwenye vyanzo vya maji zitakuwa nyingi kuliko samaki.

Hata hivyo wakati wa semina hiyo watoa mada mbalimbali wamepata nafasi ya kuelezea uwepo wa taka za plastiki na madhara yake kwa jamii ya Watanzania huku pia wakielezea hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuepusha madhara yanayotokana na uwepo wa plastiki hizo.

Kw upande wake Mhadhiri Msaidizi Shule Kuu ya Sayansi Akua na Teknolojia za Uvuvi kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam Dk.Bahati Mayoma amesema katika utafiti ambao alishiriki kuufanya mwaka 2014 moja ya matokeo ya utafiti yameonesha kuhusu athari za matumizi ya plastiki.

Amefafanua katika utafiti huo umeonesha  asilimia 20 ya samaki wamekutwa na  vipande vya plastiki ndani yao matumbo yao jambo ambalo ni hatari kwa afya.

Wakati huo huo Mkaguzi wa Mazingira wa Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam, Enock Tumbo amewaambia washiriki wa semina hiyo kuwa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 haimbani moja kwa moja mzalishaji taka za plastiki.

Ameongeza kwa kuwa sheria haibani mzalishaji,  imesababisha  mzigo wa kuondoa taka hizo za plastiki kuachwa kwa halmashauri wakati wazalishaji wapo.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad