Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema amefarijika
kuona wanufaika wa Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi wanafanyia kazi Mafunzo
hayo kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali kupitia Ujuzi waliojifunza.
Prof.
Nombo amesema hayo leo Octoba 13, Kibaha, Pwani alipotembelea banda la
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika maonesho ya Maadhimisho ya Juma
la Elimu ya Wazima yaliyoanza tangu Octoba 9 na leo ikiwa ndiyo kilele
cha maadhimisho hayo.
Akiwa katika banda la TEA, Prof. Nombo
alikutana na baadhi ya wanufaika wa Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi
yaliyotolewa kupitia ruzuku ya Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF), ruzuki
hiyo ikiwa ni fedha kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
pamoja na ufadhili wa Benki ya Dunia ambayo hadi mafunzo yanakamilika
zaidi ya Watanzania 49,000 walinufaika na mafunzo hayo.
Prof.
Nombo amesema, ni jambo la kufurahisha kuwaona wanufaika hao
wamethubutu kufanyia kazi kile walichojifunza na kuzalisha bidhaa
mbalimbali zikiwa na ubunifu mkubwa ndani yake hivyo, ni wakati muafaka
sasa waanze kuzitangaza bidhaa hizo ili kujiongezea wigo mpana wa soko.
‘‘Hizi
bidhaa mnazozalisha ni nzuri na nina uhakika zina soko kubwa tuu hapa
nchini, anadaeni mikakati ya kuzitangaza ili ziwafikie Watanzania wengi
zaidi na mwisho wa siku soko lake lizidi kukua ili muweze kufikia
malengo yenu hasa katika ujasiriamali, amesema Prof. Nombo’’
Mamlaka
ya Elimu Tanzania (TEA), imeshiriki maadhimisho ya Juma la Elimu ya
Watu Wazima kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi ambao unatoa Mafunzo ya
Ujuzi kwa lengo la kuwasaidia Watanzania kujihusisha kwenye shughuli za
uzalishaji mali ili kujikwamua kiuchumi.
Katika maadhimisho hayo ya kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima, viongozi mbalimbali walipata fursa ya kutembelea banda la TEA akiwemo Naibu Katibu Mkuu Ofisi Rais TAMISEMI anayehusika na masuala ya Elimu Bw. Charles Msonde na kujionea bidhaa zinazozalishwa na wanufaika wa Mafunzo ya SDF
No comments:
Post a Comment