HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 29, 2023

MAPEPELE AWAONGOZA WANAHABARI KUTEMBELEA MIRADI YA REGROW, HIFADHI YA NYERERE.



Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. John Mapepele, leo amewaongoza wanahabari kutembelea miradi inayofanywa na Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Nyanda za Juu Kusini (REGROW) katika Hifadhi ya Taifa Nyerere.

Akiwa hapo Bw. Mapepele amepongeza kazi nzuri inayofanywa na REGROW ndani ya Hifadhi ya Taifa Nyerere, huku akitoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuiunga mkono Serikali kwa kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.

Wanahabari hao wamejionea kasi ya ujenzi wa Kambi ya Askari wa Uhifadhi, Mtemere, geti la kuingilia na kutokea Hifadhini Kwa upande wa Wilaya ya Rufiji, Kambi ya kulala Watali/ public campsite, Nyumba za kulala Watalii na ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Mtemere.

Aidha, Mapepele amesema dhamira ya Serikali kwa sasa kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ni kufungua hazina kubwa ya utalii wa Tanzania ulio katika ukanda wa kusini kwa kutumia mradi huo.

" Tanzania imebarikiwa kuwa na hazina kubwa wa Utalii katika maeneo takribani yote nchini, kazi inayofanywa Sasa ni kuboresha miundombinu ili wageni waweze kufika kirahisi kwa kuwa kwa upande wa kaskazini wageni tayari ni wengi hivyo ni muhimu pia kugeukia upande wa kusimi amefafanua Mapepele

Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na kazi kubwa aliyofanya ya kuutangaza Utalii duniani kwa mafanikio makubwa kupitia filamu ya The Royal Tour.

Amesema kwa sasa Tanzania inapokea mafuriko ya wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuliingizia taifa mapato makubwa kupitia sekta hiyo ambapo ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini kusaidia kuutangaza utalii.

Ameongeza kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa wa kuutangaza vivutio vya Utalii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad