Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Mkoa wa Pwani wakipata maelekezo katika Kituo hicho Cha Taifa Gas.
Na Khadija Kalili Michuzi Tv
IMEELEZWA kuwa asilimia 98 ya Watanzania bado wanatumia nishati ya mkaa na kuni katika matumizi ya kupika chakula jambo ambalo linahitajika ni kuwapa elimu zaidi ya umuhimu wa matumizi ya nishati mbadala ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira.
Hayo yamesema na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Taifa Gas Ambwene Mwakalinga katika ziara ya kimafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani iliyofanyika katika kituo kikuu cha Taifa Gas kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mwakalinga ametoa rai kwa Waandishi hao kuwa mabalozi na kutoa elimu ya umuhimu kwa wananchi kutumia nishati mbadala na kuachanana na matumizi ya mkaa na kuni kwa sababu yanaharibu mazingira hali ambayo inatishia nchi kuja kugeuka na kuwa jangwa kutokana na uharibifu wa ukataji miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na kuni.
Ziara hiyo imefanyika September 6 ,2023 ambapo pia Waandishi hao wamejifunza stadi za Usalama, Afya na Ulinzi ndani ya Kituo hicho mada ambayo imetolewa na Afisa Usalama Taifa Gas Albert Gungayana amesema kuwa endapo mtu ataingia ndani ya kituo hicho hawaruhusu kubeba simu, laptops, camera ,kiberiti na hata walinzi wao hawashiki silaha kwa sababu vyote hivyo vinaweza kusababisha mripuko.
Watanzania wametakiwa kuwa makini katika namna ya kuitumia gesi kwa sababu endapo kama utaitumia ndivyo sivyo italeta madhara makubwa huku machache yaliyoainishwa ni kuto fungua mtungi na kufuatia kuwasha moto kwa sababu gesi inatabia ya kusambaa haraka huku imeshauriwa kuwa mtu uwashe kibiriti kwanza ndipo ufungue jiko na hii ndiyo iwe kanuni katika matumizi za siku zote, fungua madirisha na milango endapo utasikia harufu ya gesi ili itoke,pia usiwashe switchi ya taa kwani inaweza sababisha mripuko,unapobeba mtungi wa gesi usiulaze uusimamishe ili kukwepa madhara.
Aidha Waandishi hao wamepata fursa ya kujifunza namna mchakato mzima wa kuichayata nishati ya gesi pindi inapopokelewa hadi kujazwa katika mitungi na kuwa tayari kwa matumizi ya nyumbani.
Mwakalinga amesema kuwa wamejiwekea mikakati ya kujikita katika Wilaya zote nchini na kuwafikia wakaazi wa vijijini ili waweze kupata elimu ya matumizi ya nishati hii mbadala ikiwa ni lengo la kutunza mazingira ya nchi kwa ujumla.
"Tayari tumefanikiwa kuwakopesha majiko Mama Lishe wa Kituo Cha Msamvu Morogoro na hivi sasa wengi wao wanatumia mitungi ile ya kilo 15 na wametupa mrejesho kwamba matumizi ya mkaa kwao yalikuwa ni ghali na kujikuta wakipunguza matumizi ya fedha nyingi ambazo walikua wanatumia kununua magunia ya mkaa"amesema Mwakalinga.
Kituo hicho ni kikubwa Tanzania nzima na kazi kubwa ni kupokea gesi kutoka katika meli ambapo hupitia katika michakato husika hujazwa kwenye mitungi na kusambazwa katika Mikoa mingine mbalimbali ikiwemo nje ya nchi.
Taifa Gas ni aina ya LPG kirefu chake ni Liquidfied Petroleum Gas inayotokana na Crude Oil (mafuta ghafi),isiyo na madhara na nzuri kwa matumizi kwakuwa inakiwango kidogo cha Hydrocabons.
Taifa Gas inapatikana katika ujazo wa kilo 3,kilo6, kilo 15 na kuendelea.
Meneja Mkuu wa Kituo hicho Juma Masese amesema kuwa awali walianza kwa jina la Mihan Gas na walianza na Tani 1,440 ukilinganisha kwa sasa uzalishaji umeongezeka na kufikia Tani.7440.
Taifa Gas wana vituo 21 huku lengo letu kubwa ni kufika asilimia 100 na kila mtanzania atumie nishati mbadala pia ameongeza kwa kusema kuwa Taifa Gas wako mbioni kukamilisha ujenzi wa Kiwanda cha kutengeneza mitungi ambacho kinajengwa Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Ziara hii ni ya kwanza ambayo imeratibiwa na uongozi wa Taifa Gas na kusimamiwa na Afisa Mahusiano Ambwene Mwakalinga kwa kushirikiana na Afisa Ushirika wa Masuala ya Ndani Taifa Gas Angella Bhoke.
No comments:
Post a Comment