HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 8, 2023

WANAFUNZI 800 WAFANYA UTALII WA NDANI BUSTANI YA WANYAMAPORI YA RUHILA SONGEA

 

Na Albano Midelo,Songea

WANAFUNZI 800 wa shule mbalimbali wilayani Songea mkoani Ruvuma
wametembelea bustani ya wanyamapori ya Ruhila iliyopo mjini Songea
mkoani Ruvuma kwa lengo la kufanya utalii wa ndani.

Afisa Utalii wa Bustani ya asili Ruhila ambayo ipo chini ya Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) David Tesha amesema
wanafunzi hao walifika kutalii katika bustani hiyo katika kipindi cha kunzia
Julai hadi Agosti mwaka huu.

“Maafisa uhifadhi wa Bustani ya Ruhila wamekuwa wanapita katika shule
za msingi na sekondari mkoani Ruvuma kwa lengo la kutoa elimu ya utalii
na uhifadhi,hali hiyo imechangia idadi kubwa ya wanafunzi kila mwezi
kutembelea bustani yetu ya Ruhila’’.alisisitiza Tesha.

Amesema wanafunzi hao wakiwa katika bustani hiyo wameweza kutalii na
kujifunza mambo mbalimbali ya uhifadhi na utalii Pamoja na kufurahia
michezo ya kuendesha baskeli na michezo ya kubembea.

Hata hivyo amesema katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2023
zaidi ya watalii 3,420 kutoka ndani na nje ya nchi wameweza kutembelea
katika bustani ya Ruhila.

Amewataja watalii kutoka nje ya nchi ambao wametembelea katika bustani
hiyo kuwa wanatoka katika nchi za Japan, Sweden,Norway,Nchi za
Kiarabu,Nchi za Sikandinavia na Kenya na ametoa rai kwa watanzania
kujenga utamaduni wa kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio vya
utalii kama bustani ya wanyamapori Ruhila ambayo ipo mjini Songea.

Amewataja Wanyama ambao wanapatikana katika bustani hiyo kuwa ni
simba,pundamilia, pofu, kakakuona, kuro, swalapala, sungura,
nyumbu,jamii ya nyani ambapo amesema bustani hiyo ina madhari ya
kuvutia yakiwemo maeneo mazuri ya kupigia picha na kuweka kambi kwa
ajili ya utafiti.

Bustani ya asili ya Ruhila ambayo ipo chini ya TAWA ilianzishwa mwaka
1973 na imekuwa inapokea watalii wa aina mbalimbali kutoka ndani ya nje
ya nchi.


 Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi  wilayani Songea mkoani Ruvuma walipofanya utalii wa ndani katika bustani ya asili Ruhila mjini Songea

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad