Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NCBA Tanzania, Claver Serumaga, akionyesha uwezo wake wa kucheza golf kuelekea mashindano ya NCBA Golf Series 2023 Tarehe 30 Septemba.
====== ====== ======
Jamii ya golf nchini Tanzania imejaa msisimko tunaipokaribia Septemba 30 wakati ambapo NCBA Golf Series ya mwaka 2023 itakapofanyika. Mashindano haya makubwa zaidi kwa mwaka 2023 yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Gymkhana Golf Club ambapo wachezaji vinara wa golf nchini Tanzania watachuana kuwania nafasi tatu za kwenda kuwakilisha taifa kwenye fainali za mashindano haya Nairobi, Kenya.
Tukio hili la kipekee na lenye mvuto linatarajiwa kukusanya vipaji vya juu kabisa vya golf nchini Tanzania bila kusahau wapenzi wa mchezo huu kutoka kote nchini. Mashindano haya hayatoi tu fursa kwa nyota wa golf nchini kuonyesha uwezo wao bali pia kuacha majina yao katika vitabu vya historia ya mchezo huu.
Hayatakuwa mashindano mepesi kwani nyota wa golf watashindana katika vipengele vitatu; Mshindi wa jumla, mshindi wa jumla kwa wanaume na mshindi wa jumla kwa wanawake. Ushindi katika mashindano haya ni tiketi ya moja kwa moja kwenda kwenye fainali za NCBA Golf Series ya mwaka 2023 pale Nairobi, Kenya.
Watakapofika nchini Kenya, nyota hawa wataenda kukutana na nyota wengine kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo mashindano ya NCBA Golf Series yamepita. Washindi watatu wa jumla wa mashindano haya wataondoka na kitita cha shilingi za Kenya 100,000.
Kama hiyo haitoshi, washindi kutoka Tanzania safari yao kwenda nchini Kenya italipiwa kila kitu na Benki ya NCBA. Hii ni katika kuhakikisha kwamba wachezaji wanaifurahia safari yao na kuleata heshima kwa taifa lao.
NCBA Golf Series ni zaidi ya mashindano, hii ni sehemu ya kusherehekea umoja wetu na ushirikiano ambao tumekuwa nao kwa miaka mingi ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki. Kupitia mashindano haya benki ya NCBA inadhamiria kuendeleza ushirikiano uliopo kati yake na wateja wake.
Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania, Claver Serumaga, akizungumzia mashinfano haya, alisema, "Tuna furaha kubwa kuona vipaji na shauku ya wachezaji wa golf nchini Tanzania. Tukio hili siyo tu linaonyesha ujuzi wao lakini pia linawapa jukwaa la kuwakilisha nchi yetu kimataifa. Tunatarajia mashindano mazuri na tunawatakia kila la heri washiriki wote."
Tayari wachezaji kutoka vilabu mbalimbali vya golf nchini wameanza kujisajili ili kushiriki katika mashindano haya. Benki ya NCBA itachagua wachezaji watakaoshiriki kwenye nafasi chache zilizopo hivyo kama unatamani kushiriki mashindano haya kufanya usajili mapema.
Septemba 30 mwaka huu ndio siku ambayo viwanja vya Gymkhana Golf Club vitashuhudia vipaji vya kitanzania katika mchezo huu. Hii itakuwa mwanzo wa safari ya kuvutia kuelekea pale jijini Nairobi, Kenya kwenya fainali.
No comments:
Post a Comment