HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 16, 2023

MKUU WA JKT NCHINI AUPONGEZA MKOA WA RUVUMA KWA KUONGOZA UZALISHAJI WA CHAKULA NCHINI

 

Na Albano Midelo,Songea

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele
ameupongeza Mkoa wa Ruvuma kwa kuongoza kwa uzalishaji wa mazao
ya nafaka nchini hivyo kuchangia pato la Mkoa kwa asilimia 75.

Meja Jenarali Mabele ametoa pongezi hizo wakati anazungumza na Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas alipomtembelea ofisini kwake
mjini Songea katika ziara ya kikazi mkoani humo.

“Niwapongeza Mkoa wa Ruvuma mimi nilikuwa Mbeya wakati
mnakabidhiwa na Mheshimiwa Rais Tuzo ya mzalishaji wa kwanza wa
mazao ya nafaka nchini,katika mikoa yote ninyi mlionekana mmefanya
vizuri zaidi kwenye kilimo’’,allisisitiza.

Hata hivyo alisema anaamini Jeshi la Kujenga Taifa kambi ya Mlale
wilayani Songea ,ni sehemu ya wazalishaji wa mazao ya nafaka hivyo
katika tuzo iliyotolewa JKT Mlale pia wametoa mchango.

Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kutoa ushirikiano mkubwa
katika kambi ya JKT Mlale ambapo amemuomba Mkuu huyo wa Mkoa
kuendelea kuwatumia vijana wa JKT katika shughuli mbalimbali.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas
amesema katika msimu wa mwaka 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma
umezalishaji tani 1,598,163 za mazao ya chakula hali iliyosababisha Mkoa
kuwa na ziada ya chakula tani 1,043,525.

Hata hivyo amesema kati ya tani hizo zao la mahindi pekee zimezalishwa
tani 1,043,324 na kwamba wananchi 1,848,794 waliopo mkoani Ruvuma
wanahitaji chakula tani 554,638 hivyo Mkoa kuwa na ziada kubwa ya
chakula.

Asilimia 87 ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wanategemea kilimo.Kwa
mwaka wanne mfululizo Mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya nafaka nchini.
Mkuu wa JKT nchini Meja Jenerali Rajabu Mabele akiwa na maafisa wengine walipowasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas mjini Songea.Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas mwenye suti ya bluu kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad