Ecobank Tanzania imeshiriki pamoja na taasisi na mashirika ya Serikali na binfsi kutoka katika nchi za Kenya na Tanzania ambapo kwa mwaka huu katika Maadhimisho ya 12 ya Mara yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Hifadhi Mto Mara kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi Endelevu."
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi amesema Uhifadhi wa bonde la Mto Mara ni wa lazima na kuwataka wadau wote kushirikiana katika kuihifadhi na kulinda rasilimali hiyo muhimu.
Akihitimisha maadhimisho ya siku ya Mara mjini Mugumu wilayani Serengeti, Septemba 15,2023; Mahundi amesema bonde la Mto Mara linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinatishia uhai na uendelevu wake.
"Uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu kama vile ukataji na uchomaji miti, uchimbaji madini kwenye vyanzo vya maji, kilimo kisichozingatia sheria hizi ni baadhi ya changamoto ambazo zinakabili Mto Mara kwa upande wa Kenya na Tanzania," amesema
Amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto hizo suala la usimamizi madhubuti wa mazimgira ya bonde la mto huo kwa ujumla unahitajika na kwamba ni jukumu la kila mdau kuhakikisha bonde hilo linakuwa salama muda wote.
Naye Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Ecobank Tanzania Furaha Samalu amesema benki hiyo imeamua kujikita kwenye utunzaji wa mazingira kwani Bonde la Mto Mara linawanufaisha mabilioni ya watu katika nchi zetu hizi kwenye sekta za biashara, kilimo na utalii hivyo sote kwa umoja wetu kuanzia ngazi ya jamii hadi taifani tuna wajibu wa kutunza mazingira yake,
Pia amesema Ecobank Tanzania wameshiriki maadhimisho hayo miaka 12 ili kuweza kueleza huduma wanazozitoa kwa wadau mbalimbali ili benki hiyo iweze kujipanua na kuendelea kusaidia katika suala zima la utunzaji wa mazingira ya bonde hilo.
Ecobank Tanzania imeweza kutoa elimu kwa jamii ikiwemo mashuleni hasa kwenye shule za Sekondari na msingi za Mugumu na Halmashauri ya Serengeti ili kujenga uelewa wa utunzaji na kuhifadhi mazingira ikienda sambamba na kujua huduma zinazotolewa na banki hiyo.
Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Ecobank Tanzania Furaha Samalu(kulia) kuhusu na mna walivyojikita katika kutunza mazingira pamoja na kazi zinazofanywa na benki hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mara yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Hifadhi Mto Mara kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi Endelevu."
Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau kutoka taasisi na mashirika ya Serikali na binfsi kutoka katika nchi za Kenya na Tanzania ambapo kwa mwaka huu katika Maadhimisho ya 12 ya Mara yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Hifadhi Mto Mara kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi Endelevu."
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Ecobank Tanzania Furaha Samalu(kulia) akipanda mti wakati wa Maadhimisho ya 12 ya Mara yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Hifadhi Mto Mara kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi Endelevu."
No comments:
Post a Comment