Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba ameshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Elimu na Maendeleo unaofanyika nchini Uingereza kuanzia tarehe 12 - 14 Septemba, 2023.
Mkutano huu unajulikana kama UKFIET International Conference on Education and Development.
Katika Mkutano huo Dkt. Komba ameshirikiana na Bi. Joan Minja kuwasilisha juu ya utekelezaji wa Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo katika maeneo ya msawazo wa walimu na usambazaji wa vitabu vya Kiada na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia.
Aidha, mkutano huo umehudhuriwa pia na Dkt. Charles Msonde Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bwana .Kayode Sanni Kiongozi wa Timu Mradi wa Shule Bora na Bwana.Benjamini Oganga,Kiongozi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Elimu(System Strengthening Lead)
Thursday, September 14, 2023
Home
Unlabelled
MKURUGENZI TET ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA ELIMU NA MAENDELEO NCHINI UINGEREZA
MKURUGENZI TET ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA ELIMU NA MAENDELEO NCHINI UINGEREZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment