Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Ndugu Elias M. Kayandabila amemtaka Mkuu wa Kitengo cha Taka Ngumu Ndugu Adamu Baleche kuhakikisha kuwa ndani ya siku tatu awe ameondosha taka zote zilizopo maeneo yote ya kukusanyia taka na kuzipeleka dampo.
Kanyandabila
ameyatoa maelekezo hayo leo Septemba 18, 2023 wakati wa Ziara fupi ya
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT) ya kukagua hali ya usafi katika
viunga vya Manispaa ya Tabora.
Aidha Ndugu Kayandabila ameunda
timu ndogo itakayoshirikiana na Kitengo cha Taka Ngumu katika kuratibu
na kusimamia kazi zote za usafi mjini hapo, lengo kubwa ikiwa ni
kuongeza ufanisi wa shughuli za usafi katika Manispaa yetu.
Wajumbe
wa CMT nao baada ya kujionea hali mbaya katika maeneo ya kukusanyia
taka, wameafiki kwa pamoja umuhimu wa timu hiyo ndogo ambayo itaongeza
nguvu kwenye kitengo cha taka ngumu.
No comments:
Post a Comment