HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 26, 2023

Mfumo wa Manunuzi TANePS kufungwa

 


*PPRA yaongezewa meno Ripoti yake ya Manunuzi ya Umama kukabidhiwa kwa Rais

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SERIKALI katika kuendelea kuboresha mifumo ya TEHAMA Nchini Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) umetangaza rasmi kuufunga mfumo TANeps ifikako Septemba 30 hivyo ametoa rai kwa taasisi zote za umma kujiunga kwenye mfumo mpya wa manunuzi wa kielekroniki wa Taifa ufahamikao kama e-Procurement System of Tanzania (NeST).

Hayo ameeleza jana na Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Eliakim Maswi, wakati akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya habari kuhusu maboresho ya mfumo huo na kuachana na wazamani ambao haukuwa salama.

Alisema baada ya Serikali kufanya tathmini ya kina ya mfumo uliopo wa TANePS wataalamu walishauri kujengwa kwa mfumo mpya ajili ya kupata ufumbuzi wa changamoto kwani mfumo ulipo sasa haukidhi mahitaji ya Serikali.

Alisema Mfumo wa NeST utakuwa na uwezo wa kuongeza uwazi na uwajibikaji na utakidhi mahitaji ya sheria za nchi, taratibu na miongozi ya ununuzi.

"Lakini pia kuwa na mfumo wa NeST unakwenda kupunguza mianya ya rushwa na kuleta thamani halisi ya fedha za Serikali katika ununuzi wa umma," alisema

Aidha aliongeza kuwa timu ya wataalamu iliishauri Serikali ianze kazi ya kujenga mfumo mpya pamoja na kutatua changamoto zilizopo kwenye mfumo uliopo.

Maswi, alisema kuwa hadi kufikia Juni 2023 taasisi nunuzi 864 zimesajiliwa kwenye mfumo na ndio zilizopaswa kutumia mfumo huoambapo wazabuni 37, 445 wamesajiliwa kwa ajili ya kutumia mfumo.

Alisema tangu kuanza kutumia mfumo zaibuni 142,606 zilitangazwa kwa kutumia mfumo wa zabuni zilizoendela hadi kupata tuzo kwa kutumia mfumo ni 26,366 sawa na asilimia 18.5 na hivyo kuonesha kiwango kidogo katika kukamilisha mchakato wa ununuzi kwa kutumia mfumo huo.

Kati ya zabuni zilizotangazwa zaidi ya asilimia 81.5 ya zabuni hizo hazikumaliza mchakato wake kwa kutumia mfumo. Wakati mfumo wa sasa wa NeST ni rahisi na unatumia dakika 30 na umeunganishwa na taasisi zote ikiwemo Brela taasisi hivyo PPRA ataweza kuona kila kitu kwa wakati huohuo jambo ambalo litaleta ushindani wa kweli na wa haki.

“Tunajua wapo waliokuwa wakiomba zabuni maana halisi ya zabuni kuomba mtandaoni ni kupunguza na kuondoa kabisa rushwa lakini kupitia mfumo huu mpya mengi tunayaona kwa wakati na hata kuweza kuwasiliana na wahusika kama kuna jambo ambalo haliko sawa,” alisema Maswi.

Alisema mfumo wa NeST utasaidia kudhibiti rushwa, mchakato wa zabuni kuchelewa na kuongeza uwazi wa zabuni.

Alisema taasisi zinazosimiwa na Msajili wa Hazina na Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (TAMISEMI), zinapaswa kuanza kutumia mfumo mpya kwa shughuli za ununuzi wa umma na kwamba itakapofika Oktoba Mosi mwaka huu taasisi nunuzi zote za serikali hazitaweza kutuma mialiko ya zabuni katika mfumo wa zamani wa TANePS.

Maswi amesema kuwa PPRA imeongezewa meno kwani ripoti yake inapeleka moja kwa moja kwa Rais kama ilivyo Ripoti ya CAG na Takukuru hali itafanya ununuzi wa umma kuleta tija.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad