Waziri wa Madini,
Anthony Mavunde, ameipongeza Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd
kwa kufungua ofisi mkoani Geita na kuona umuhimu wa kushirikiana na
sekta ya madini hasa wachimbaji katika kuwapatia vifaa.
Kampuni
hiyo imezindua ofisi iliyopo katika Soko Kuu la Dhahabu Geita na
kukabidhi maroli matatu yaliyonunuliwa na wachimbaji katika wakati hu wa
maonyesho ya Madini yanayoendelea mkoani humo.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo, Mavunde amesema itarahisisha shughuli za uchimbaji
ili Watanzania washiriki kikamilifu katika sekta ya madini.
“Nawapongeza
kwa kuamua kusogeza huduma karibu kabisa na wachimbaji, niwaombe
muendelee kutanua wigo, wachimbaji ni waaminifu wanao uwezo mkubwa wa
kuchukua mitambo kwa njia ya mkopo na kuirejesha,” amesema Mavunde.
Amesema
pia mwaka huu Mkoa wa Geita umewekewa lengo la kukusanya maduhuli ya
Serikali Sh bilioni 243 na ndiyo mkoa unaoongoza kwa mchango mkubwa wa
maduhuli.
Mkurugenzi
wa Masoko na Biashara wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd ,
Salman Karmali, amesema GF imepanga kuwafikia watanzania woote katika
kanda tofauti na kwa kuanzi awameamua kufungua ofisi katika kanda ya
ziwa itakayorahisihia wafanyabiashara na wadau a madiki kupata huduma
zetu kwa uharaka
Pia Salman alisema hii yote ni matunda mazuri ya
serikali ya awamu ya 6 kwa kuweza kuweka mazingira mazuri kwa
wawekezaji na kampuni hii kwa mwaka huu inalengo la kufanya uzalishari
wa magari makubwa (trucks) kufikia magari 1,500 yanayounganishwa
katika kiwanda chetu cha GFA kilichopo Kibaha mkoani Pwani na hizi gari
tunazokabidhi kwa wateja hii leo ni ni ni gari zilizotengenezwa nchini
Tanzania.
GF waliingia makubaliano na Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) ambalo lina vifaa vya kuchoronga na kufanya tafiti huku
kampuni hiyo ikitoa mashine na maroli.
Aidha
amesema ku[itia mkataba huo GF itaweza kuwap[atia mitambo na maroli
wachibaji wadogo na wakubwa ilik kuwakomboa chini ya usimamizi wa
STAMICO
Mkurugenzi wa STAMICO amesema miongoni mwa mambo
waliyokubaliana ni kusogeza huduma sehemu za wachimbaji na kuwauzia au
kuwakodishia vifaa.
“Tukio hili ni utekelezaji wa mambo ambayo tulikubaliana, jambo lingine tulilokubaliana ni kukodisha vifaa pamoja na kuuza.
“Sekta ya madini inahitaji mtaji mkubwa au uwekezaji mkubwa, lakini inahitaji muda mrefu.
Ukimuangalia
mchimbaji mdogo si lazima awe na resource (rasilimali) nyingi, anaweza
akachimba bila kuwa na uwekezaji wa muda mrefu.
“Kwahiyo tukaona
tukae pamoja tujadiliane tuone namna ya kumrahisishia mchimbaji mdogo
asipate presha ya kuwa na mtaji mkubwa wa kumiliki trucks, bludoza ndio
aweze kuchimba,” amesema.
Meneja wa Benki ya CRDB Geita, Efrosina
Mwanja, amesema wanashirikiana na kampuni hiyo kuwakopesha wachimbaji
magari na vifaa.Kwa mujibu wa Meneja huyo kupitia makubaliano hayo
mchimbaji anayehitaji gari au vifaa kazi hutakiwa kuchangia asilimia 30
ya gharama kisha asilimia 70 hukopeshwa na benki hiyo.
“Tunawakopesha
Watanzania, mfanyabiashara au mchimbaji, atachangia asilimia 30 ya
gharama yote ya manunuzi ya gari au vifaa. Kwahiyo tunatoa asilimia 70
ya gharama zote na dhamana ni kile chombo ulichonunua,” amesema Mwanja.
Amesema
pia wamekuwa wakiwapeleka wachimbaji wadogo nje kama vile China, Dubai
na Uturuki kwa lengo la kujifunza na kupata ufanisi katika shughuli za
madini.
Katika hafla hiyo kampuni hiyo ilitoa tuzo kwa wadau
mbalimbali akiwemo Waziri Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Geita kutambua
mchango wao katika kuendeleza shughuli za kampuni hiyo.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi za Kampuni ya GF Trucks & Equipment mkoani Geita.
Mavunde akiwa katika Picha ya Pamoja na wateja pamoja na voiongozi wa kampuni ya GF
Waziri wa Madini, Anthon Mavunde akiwakabidhi wateja wengine
No comments:
Post a Comment