HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 6, 2023

MADHIMISHO YA MIAKA 50 YA USTAWI WA JAMII KUAMBATANA NA KUTOA ELIMU NAUSHAURI

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Dotto Biteko Leo katika Mkutano wa Maafisa Ustawi wa Jamii unaofanyika katika Ukimbi wa Venance Mabeyo Dodoma Kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.Philip Isdor Mpango amezindua maadhimisho ya miaka 50 ya uwepo wa Chuo cha Ustawi wa jamii, ikiashiria Kuanza kwa shughuli Kuelekea Kilele cha maadhimisho hayo  Disemba 06, 2023. 

Maadhimisho hayo yataambatana na utoaji elimu na ushauri katika maeneo mbali mbali ya Nchi ambapo kuanzia Tarehe 8 mpaka 10 Septemba 2023 , Chuo cha Ustawi wa Jamii kitapiga kambi Katika Viwanja vya Nyerere Square ambapo huduma za Msaada wa kisaikolojia Ushauri wa kisaikolojia, Ushauri wa mahusiano na ndoa, elimu ya afya ya uzazi kwa vijana, elimu na ushauri wa malezi na makuzi ya watoto na vijana, elimu na ushauri kuhusu sheria za kaz na afya ya akili hii ikiwa ni sehemu ya kwanza ya ratiba za  elimu na huduma za maadhimisho kuelekea Kilele Disemba 2023.
Mkuu wa Chuo Ustawi wa Jamii akizungumza kabla ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii.

Watumishi Wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Wakiongozwa na Mkuu wa chuo hicho Dkt. Joyce Nyoni Wakati wa Mkutano wa Maafisa Ustawi wa Jamii Dodoma Wakifuatilia Mkutano huo kabla ya Uzinduzi wa Maadhimisho Ya Miaka 50 ya Chuo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad