RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi kuanzia tarehe 15 - 20 Septemba, 2023. Katika ziara hiyo ya mikoa ya kusini, Rais Samia atazindua na kukagua miradi mbalimbali pamoja na kusikiliza kero na matatizo ya wananchi.
Rais Samia pia atazindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini, kuzindua Chujio la Maji Mangamba, atakagua uwanja wa ndege na pia kuzindua barabara mkoani Mtwara.
No comments:
Post a Comment