HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 7, 2023

WENZA WA VIONGOZI WAZINDUA HUDUMA ZA TAULO ZA KIKE MASHULENI

Mama Zakhia Bilal akigawa taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtoni wilayani Temeke. (Picha kwa hisani ya Manispaa ya Temeke). Wenza wa viongozi wakiongozwa na Mama Tunu Pinda (wa kwanza kushoto) na Mama Mary Majaliwa (wa tatu kutoka kushoto mstari wa mbele).

Watoto wa moja ya Shule nane za msingi  Wilayani Temeke zilizoshiriki kwenye kongamano la maadili lililoandaliwa na Asasi ya wenza wa viongozi ya Ladies of New Millenium wakimkabidhi risala yao mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mheshimiwa  Mobhare Matinyi  anaye shuhudia  ni Mama Mary  Majaliwa.
Baadhi ya wanafunzi  waliohudhuria katika kongamano hilo  la  mafunzo  ya maadili kwa watoto wa kiume  lililofanyika kwenye ukumbi wa Sabasaba Wilayani Temeke, Dar es Salaam.

Na Khadija Kalili Michuzi Tv
ASASI ya wenza wa Viongozi nchini iitwayo 'Ladies of New Millenium', leo Agosti 7, 2023, imezindua mradi wa choo kwa ajili ya kusaidia watoto wa kike ili waweze kujisitiri na kupata huduma zote wanazozihitaji wakiwa kwenye hedhi.

Uzinduzi huo umefanywa na mlezi wa Asasi hiyo, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mheshimiwa Mobhare Matinyi katika Shule ya Msingi Mtoni, Wilayani Temeke.

Mheshimiwa Matinyi ametoa shukrani za dhati kwa taasisi hiyo kwa kukikarabati choo cha watoto wa kike na kuwezesha kupata huduma hiyo muhimu.

Mheshimiwa Matinyi amewashukuru pia wadau mbalimbali akiwemo Bi. Celina Godfrey Retala, Afisa Mtendaji Mkuu wa HQ Pads kwa kuchangia katoni 100 za taulo za kike kwa ajili ya watoto kujihifadhi wakati wa hedhi.

DC Matinyi ametoa wito kwa watu na wadau wengine kuunga mkono juhudi hizi ili kumuwezesha mtoto wa kike kupata elimu bora bila usumbufu na kuleta mafanikio hapo baadaye kwa jamii.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mtoni, Wilayani Temeke, Victor Kangati, ameipongeza Asasi hiyo kwa kuleta mradi huo kwani ni miongoni mwa mbinu kubwa zinazosaidia kupunguza utoro kwa watoto wa kike shule.

Taasisi hiyo yenye lengo la kuwawezesha vijana na watoto kupitia elimu yenye ufanisi na ujumuishwaji katika ngazi zote za maamuzi, imeendesha hafla hiyo na kuhudhuriwa na wake wa viongozi akiwemo mlezi wa taasisi, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa, Mwenyekiti wa taasisi Mama Tunu Pinda na wenza wengine wa viongozi wakiwemo Mama Zakhia Bilal, Mama Asha Bilal, Mama Asina Kawawa na Mama Asha Balozi na Mama Mwantumu Mahiza na Wadau wengine wa maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan Foundation, HQ Pads, na Tosh Cargo .
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi akizungumza  kwenye  kongamano la  mafunzo ya maadili kwa watoto wa kiume  wa shule za msingi  lililoandaliwa na Asasi  ya wenza wa viongozi  nchini iitwayo Ladies of New Millenium.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Mobhare Matinyi, akimshukuru Mama Celina Retala, Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha HQ Psds cha taulo za kike kilichopo wilayani Temeke. (Picha kwa hisani ya Manispaa ya Temeke).
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akikata utepe kuzindua mradi wa ukarabati wa vyoo vya wasichana na uwekaji wa taulo za kike katika Shule ya Msingi Mtoni wilayani Temeke. (Picha kwa hisani ya Manispaa ya Temeke).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad