Na Mwandishi Wetu
WANAMITINDO
wanne kati ya 200 waliojitokeza kwenye usahili wa Shindano la Future
Face 2023 wameteuliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye chaguo la awali la
Future Face duniani 2023.
Usahili wa Shindano hilo la Future Face
umefanyika kwa kushirikiana na kuratibiwa na Mwanamitindo wa kimataifa
Millen Happiness Magese umefanyika jijini Dar es Salaam huku majaji wa
nne wakihusika katika kuchuja wanamitindo waliojitokeza hadi kubakia na
wawakilishi wanne kati ya hao 200 waliojitokeza.
Majaji katika
usahili wa shindano hilo la kimataifa ambalo ndio mara ya kwanza
kufanyika nchini Tanzania walikuwa Ally Rehmtullah, Mwanamitindo wa
Kimataifa Millen Happiness Magese, Martin Kadinda na Jamilla Vera Swai.
Akitangaza
matokeo ya usahili huo Mwanamitindo wa Kimataifa Millen Happiness
Magese amesema kuwa vijana zaidi ya 200 walitokeza kwenye usahili
uliofanyika mwishoni mwa wiki lakini baada ya kuangalia sifa na vigezo
vya Shindano hilo wamefanikiwa kuwapata wawakilishi wa nne ambao hao
watachuana tena na kumpata mmoja ambaye ataiwakilisha nchi ya Tanzania
katika mashindano hayo.
Amewataja walioteuliwa kwenye usahili huo
ni Rachel Amani Julius(20) - 5’8 Ft, Joyceller Lasway(25l - 5’9 Ft,
Neema Evaresty(23) - 5’11 Ft pamoja na Jasinta David Makwabe(25) - 5’11
Ft.
Mwanamitindo wa Kimataifa Millen Happiness Magese amesema
baada ya kupatikana kwa wawakilishi hao hakutakuwa na kambi huku
akifafanua yule atakayechaguliwa kuiwakilisha nchi Septemba mwaka huu
atakwenda nchini na Nigeria na akifanikiwa kushinda anakwenda nchini
Paris au Italy.
"Nawashukuru majaji wote kwa ushiriki na kujitoa
kwao kufanikisha jambo hili muhimu ambalo limeandika historia kubwa
katika nchi yetu kwani ndio mara ya kwanza Shindano la Future Face
linafanyika nchini Tanzania.
" Pia nawashukuru sana vijana wote
kwa kujitokeza kwa wingi, sikutegemea kuona umati uliojitokeza na Kama
mtu hakuweza kufika basi anaruhusiwa kutuma maomba yake kwa njia ya
mtandao kupitia www.futurefaceglobal.com ambapo mwisho ni Septemba 22,
2023" amesema.
Aidha amevishukuru vyombo vya habari nchini
Tanzanka kwa kuendelea kutoa ushirikiano hasa katika kuripoti kuhusu
shindano hilo la kimataifa kila hatua inayofanyika ikiwemo ya usahili
huo.
Kuhusu walioteuliwa amesema wawe washindani kwamba wakubali
kushinda au kushindwa. Pia kushindwa waichukulie kama sehemu yao
kuendelea kujaribu tena hasa kwa kutambua mashindano hayo ni makubwa na
yanaangaliwa na mamilioni ya watu duniani kote.
Awali wakati
anazungumzia Shindano hilo, Mwanamitindo wa Kimataifa Millen Happiness
Magese amesema ameshirikiana na Future Face kuleta Shindano hilo
kubwa zaidi la kimataifa la kusaka wanamitindo mwaka wa 2023.
Amesema
Shindano hilo ni la kipekee lililoandaliwa na Wakala mkubwa zaidi wa
wanamitindo barani Afrika, Beth Model Management na limekuwa linajivunia
utofauti wake wa ukubwa, umri, rangi na kabila, na ulemavu, huku
shindano likiwa na sera ya fursa sawa.
Wawakilishi
wanne walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika hatua ya awali ya
Shindano la Future Face Kimataifa 2023 wakiwa kwenye pich ya pamoja
baada ya kutangazwa kushinda usahili uliohusisha vijana zaidi ya 200
uliofanyika jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment