Na Mwandishi wetu, Dodoma
Wagombea
58 kutoka vyama 17 vya siasa vyenye usajili kamili wameteuliwa na Tume
ya Taifa ya Uchaguzi kuwania nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo la
Mbarali lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na kata sita za
Tazanzania Bara.
Tarehe 05 Agosti, 2023 Tume ilitangaza uchaguzi
mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara na uteuzi wa
wagombea umefanyika tarehe 19 Agosti, 2023, kampeni zimeanza tarehe 20
Agosti 2023 na zinatarajiwa kuhitimishwa tarehe 18 Septemba, 2023 ambapo
uchaguzi utafanyika tarehe 19 Septemba, 2023.
Fomu za uteuzi wa wagombea zilitolewa kuanzia tarehe 13 hadi 19 Agosti, 2023 ambapo jumla ya wagombea 70 walichukua fomu.
Kati
ya wagombea 70 waliochukua fomu, wanawake walikuwa 21 na wanaume
walikuwa 49. Kati ya wagombea 58 walioteuliwa wanawake ni 14 na wanaume
ni 44.
Wagombea hao
wametoka kwenye vyama 17 ambavyo ni; CCM, AAFP, ACT – WAZALENDO, TLP,
NRA, SAU, ADA – TADEA, ADC, CCK, CUF, DEMOKRASIA MAKINI, DP, NCCR –
MAGEUZI, NLD, UDP, UMD na UPDP.
Kata
zitakazofanya uchaguzi mdogo ni; Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la
Dodoma, mkoani Dodoma, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya
Misungwi, mkoani Mwanza, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya
Wilaya ya Moshi na Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya
Rombo, mkoani Kilimanjaro, Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya
Madaba na Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani
Ruvuma.
Wagombea
na wafuasi wao wakiangalia fomu za uteuzi zilizowekwa wazi na Msimamizi
Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la
Dodoma. Uteuzi ulifanyika Agosti 19,2023 ambapo uchaguzi katika Jimbo la
Mbarali na Kata sita za Tanzania bara unataraji kufanyika Septemba 19
mwaka huu. (Picha na NEC).
Msimamizi
wa Uchaguzi Jimbo la Mbarali Bw.Missana Kwangura akibandika fomu za
uteuzi za vyama kumi na tatu vilivyoteuliwa kugombea ubunge katika
uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbarali mkoani Mbeya. (Picha na NEC).
No comments:
Post a Comment