HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 22, 2023

UCHAGUZI MKUU 2020 HAUKUA NA HALI NZURI YA DEMOKRASIA, KWA SASA IMEIMARIKA

 


"UCHAGUZI mkuu wa 2020 haukuonesha hali nzuri ya demokrasia kwani vyama vya upinzani vilipata viti nane tuu vya upinzani ambapo Tanzania bara vilipata wabunge wawili kati ya viti 264 hali ambayo mwanzo haikuwa hivyo."

Hayo yamesemwa leo Agosti 22,2023 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Ibrahim Lipumba wakati akifungua Mkutano wa kitaifa wa wadau kujadili hali ya Demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na Vitongoji 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025. Amesema kuwa hadi sasa Tanzania haijafanikiwa kujenga demokrasia ya kweli.

Licha ya hayo amesema kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto za kujenga uchumi na kujenga misingi imara ya kidemokrasia.

Prof Lipumba amesema kuwa Demokrasia ni adili la vyama vyote na hakuna mwananchi yeyote mwenye hati miliki ya nchi hii.

Aidha Prof. Lipumba ametoa wito kwa balozi zote kushirikiana na TCD katika kukuza demokrasia nchini huku wakihifadhi mazingira.

Awali Prof. Lipumba amesema kuwa kesho Agosti 23, 2023 katika mkutano huo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ambapo naye atazungumzia kuhusiana na Demokrasia nchini.

Akizungumzia Swali tathmini ya hali ya demokrasia nchini Joseph Selasini amesema kuwa Demokrasia inashuka kwa sababu uchaguzi unasimamiwa na upande mmoja pia unasimamiwa na watendaji wa serikali na wanachama wa chama fulani.

"Kwa sasa tunaenda kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, wangapi tunajua kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa hauna sheria bali unasimamiwa na TAMISEMI ambaye pia ni mchezaji." Amesema

Kwa upande wa katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, John Mnyika amesema kuwa ili nchi ielekee kwenye mkondo wa kidemokrasia lazima kuandika katiba mpya kwa sababu katiba ya mwaka 1977 iliandikwa kwa chama kimoja na Chama cha dola.

Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulahaman Kinanaamesema kuwa demokrasia nchini imekuwa licha yakuwa na mapungufu katika sheria na kusimamia sheria wakati wa uchaguzi. Akitoa ulinganifu amesema idadi ya wawakilishi wa vyama inaongezeka katika bunge. Japo kuna kasoro, lakini dhamira ya kurekebisha sheria ya Uchaguzi ipo hivyo kutakuwa na uchaguzi huru na haki mwaka 2024/25.

Akizungumzia uhuru wa kuzungumza pia kinana amesema kuwa upo lakini kila uhuru una mipaka yake. Uhuru bila nidhamu ni wendawazimu, nidhamu bila uhuru ni utumwa.

Kwa Upande wa Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema kuwa hali ya sasa inahitaji mazungumzo ya kitaifa kuimarisha makubaliano ya kitaifa. Ingawa wadau wanaweza kutofautiana katika mitazamo, wanaweza kukubaliana kuhusu maslahi ya kitaifa. 

Amesema TCD inaendesha mkutano wa wadau kujadili demokrasia na uchaguzi, kufuatia juhudi za Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Mkutano wa awali wa TCD ulijadili marekebisho ya uchaguzi, matokeo yake yalipendekeza marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Vyama vya Siasa, na kuimarisha ushirikiano wa vyama vya siasa. 

"Mkutano wa wadau wa kitaifa utalenga kukuza demokrasia katika nchi. Malengo yake ni kujenga jukwaa la mazungumzo, kujadili mafanikio na changamoto za demokrasia, kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa awali, na kutoa mapendekezo kwa mustakabali.
Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza katika leo Agosti 22, 2023 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, katika Mkutano wa kitaifa wadau kujadili hali ya Demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na Vitongoji 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD), Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza leo Agosti 22, 2023 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, katika Mkutano wa kitaifa wadau kujadili hali ya Demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na Vitongoji 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Demokrasia Tanzania, Bernadetha Kafuko akizungumza leo Agosti 22, 2023 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, katika Mkutano wa kitaifa wadau kujadili hali ya Demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na Vitongoji 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Wazungumzaji wa awamu ya kwanza katika Mkutano wa kitaifa wadau kujadili hali ya Demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na Vitongoji 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Baadhi yawanachama wa vyama mbalimbali vya siasa wakiwa kwenyeMkutano wa kitaifa wadau kujadili hali ya Demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na Vitongoji 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad