Fundi Simu Eunice Kavishe akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore kuhusiana na umhimu wa kujifunza kwa ujuzi , jijini Mbeya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akipata maelezo kuhusiana na urembo unaendeshwa na baadhi ya vyuo vya VETA katika Banda la VETA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.Na Chalila Kbuda , Michuzi TV Mbeya
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema katika utoaji wa elimu ya mafunzo stadi inakwenda kwenye kutoa uzalishaji wa vijana na wanawake wataokuwa wazalishaji katika sekta ya kilimo.
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo CPA Anthony Kasore wakati alipotembelea banda lake VETA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
CPA Kasore amesema kuwa katika kufanikisha uzalishaji wa vijana wenye ujuzi serikali imeendelea kujenga vyuo katika kila wilaya ili vijana hao wakiingia kwenye kilimo kinakuwa na tija kutokana zana ambazo zinabuniwa na walimu na wanafunzi kutokana na mahitaji katika eneo la chuo kilichopo.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu Kasore amesema katika maonesho Nane Nane VETA kupitia walimu na wanafunzi wamebuni nyenzo za rahisi za kutumia katika kilimo kwa gharama nafuu.
"Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan imeweka fedha nyingi katika ujenzi wa vyuo ufundi ni matumani yake watendaji wake kutekeleza dhamira ya Rais kwa vitendo"amesema CPA Kasore.
Aidha amesema kuwa vyuo vilivyojengwa vijana waende kusoma na kupata ujunzi kutokana na kuwepo kwa uwekezaji wa viwanda nchini ambavyo vinahitaji asilimia 90 ya nguvu kazi yenye ujuzi wa kuhudumia viwanda hivyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akizungumza katika Banda la VETA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akipata maelezo katika mtambo wa usindikaji wa maziwa katika Banda la VETA kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Mwalimu wa Urembo VETA Shinyanga Judy Mwita akitoa huduma ya unyoaji katika banda la VETA.
No comments:
Post a Comment