HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 2, 2023

KAMPUNI YA GF YAZINDUA GARI YA FORLAND NANENANE MBEYA

 


Kampuni ya Gf trucks & Equipment’s Ltd imetambulisha sokoni gari mpya aina ya FORLAND Ikiwa ni maaalumu kwa shughuli za Kilimo na usafirishaji wa Mazao kutoka sehemu moja hadi kungine

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Gar hizo aina ya FORLAND afisa masoko na mauzo wa kampuni hiyo, Peter Wiliam lisema kampuni wamesikia klilio cha muda mrefu cha wakulima kwani sio kila mmoja anauwezo wa kununua magari makubwa tan 17 kutokana na shughuli husika sisi tukaamua kuwalete magari mapya kabisa 0 kilometa .

Gari hizi za FORLAND ni miongoni mwa magari yaliyo unganishwa katika kiwanda chetu cha GFA kilichopo Kibaha mkoani Pwani na hivyo bei zetu ni nafuu mmno ukilinganinsha na hapo awali ambapo tulikua tunhaangza magari kutoka nje.

Shughuli za kutoa mazao shambani zinahitaji gari yenye ukubwa wa wastani sasa sisi tumeamua kuwaletea gari mpya kabisa aina ya Forland kwa ukubwa tofauti yaani kuanzia tan 1.5 , tan 2 hadi tani 17 kutegemea na mahitaji husika
Pia wameamua kuja kuzindulia huku kutokana ukanda huu wa Nyanda za juu kusini hasa ndio kilimo cha ,Mahindi ,Mpunda na sasa hivi Parachichi zinapatikana kwa wingi hivyo ni busara kuungana na dserikali kuamua kuwasogezea huduma karibu.

Kampuni ya GF imeekuwa namba moja kwa uuzaji wa mitambo aina ya XCMG kwa shughuli za Migodini na wakandarasi kwa ajili ya uchongaji wa barabara

Nae Mfanya biashara wa kilimo, Atupele Mwakalinga aliwashukuru GF kwa kuwakumbuka na kuamua kuja kuzindulia gari hizo katika mkoa wa Mbeya wakati huu wa Maonyesho ya kilimo na kucha utamaduni wa kila kitu kuzindulia Dar es salaam hata kama wahitaji wa kuu wa bidhaa ahizo wanapatikana huku mikoani

Kampuni ya GF kwa kushirikiana na Taasisi za Kibenki imeanzisha utaratibu nafuu wa kumwezesha mkandarasi mzalendo (mtanzania) na mwenye mradi mkononi kuweza kumkopesha Mitambo na mashine kwa vigezo na mashariti ilim kuweza kushindana na makampuni ya kigeni
Afisa Mauzo wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Peter William akiwaezea ubora wa magari ya mizigo ya FORLAND kwa ajili ya shughuli za kilimo wakati wa Uzinduzi wa gari hizo katika viwanja vya maonyesho ya Nane nane jijini Mbeya .

Wateja wakiangalia Ubora wa gari ya FORLAND wakati uzinduzi wa gari hiyo uliofanyika wakati wa maonyesho ya Kilimo kwenye viwanja vya Nanenane jijini Mbeya .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad