Na Mwandishi Wetu
KWAYA maarufu nchini ya Gethsemane inayosali Kanisa la wasabato Kinondoni, ipo mbioni kutoa video ya wimbo wake mpya unaofahamika Dunia hii.
Taarifa iliyotolewa leo Agosti 13, 2023 jijini Dar es Salaam na uongozi wa Kwaya hiyo yenye makazi yake Kinondoni imesema video hiyo imegusa uhalisia wa maisha katika Dunia tunayoishi. Video hiyo imefanywa na Director Joowzey.
Pia video ya wimbo huo ambayo itatoka Jumamosi ya wiki hii itakuwa kwenye albam yao ya Bado Kitambo, ambayo nyimbo zake zimeendelea kujizolea umaarufu na kupendwa na wapenzi na mashabiki wa muziki wa Injili.
"Mnaweza kuuliza lengo la wimbo ni nini? Jibu; lengo ni kuwaambia watu kuwa Mungu anatoa faraja kwa watu wote wanaopitia Mapito/ shida mbalimbali na changamoto za dunia.
"Na video ya wimbo huo tunaitumia kama zawadi kwa mashabiki wetu wa nchini Kenya kwani kwaya yetu wiki hii yote na wiki ijayo tupo Kenya tukiendelea kuhudumu kwa Nyimbo Kwenye mikutano ya Injili, (Makambi) " imesema taarifa hiyo.
Kuhusu Mipango ya Gethsemane imesema pamoja na mambo mengine wanayoendelea kuyafanya wanatarajia kuzindua album yao ya Bado Kitambo mwishoni mwa mwaka 2023.
No comments:
Post a Comment