HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 11, 2023

Vyuo vya Afya Nchini vimetakiwa kuzingatia kanuni na miongozo- Kaimu Katibu Mtendaji Makota

 

Mkurugenzi wa Udahili, Utahini na Utunuku, Dkt. Marcelina Baitilwake akizungumza kuhusiana na vyuo vya  kada ya afya kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa , jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vyuo Binafsi vya Afya nchini (APHCOT) Dkt. Joel Limbu Maduhu akizungumza kuhusiana na umhimu wa mkutano katika kujenga uimara wa kada ya afya nchini kwa vyuo vya afya , jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa mkutano kati ya NACTVET na  wakuu wa Vyuo vya Afya uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mtendaji, Dkt. Amani wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) akizungumza wakati akifungua mkutano wa  Kamati ya Udahili wa  pamoja uliohudhuriwa na Wakuu wa Vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi, Wizara ya Afya, APHECOT na wawakilishi wa Mabaraza ya kitaaluma kwenye kada za Afya uliofanyika jijini NACTVET - Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limewataka Wakuu wa Vyuo vya Afya nchini kuzingatia kanuni, miongozo na maelekezo ya NACTVET wakati wa mchakato wa udahili ili kupunguza changamoto zinazojirudia wakati wa udahili wa Pamoja.

Dkt. Makota ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Wakuu wa Vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi, Wizara ya Afya, APHECOT na Wawakilishi wa Mabaraza ya kitaaluma kwenye kada za Afya uliofanyika Ofisi za NACTVET jijini Dar es Salaam.

Dkt. Makota amwakumbusha wa wakuu wa vyuo hao kwamba mifumo wa Udahili wa pamoja ni njia muafaka ya kudahili na wale wanaotaka kusomea masuala ya afya na unapaswa kufuatwa kwa uadilifu na vyuo vyote vya afya ili kuiwezesha NACTVET kuchakata maombi yote kwa uhakika na kwa wakati.

Amesema kuwa NACTVET ni kusimamia kwa kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi viwango vilivyowekwa katika sera na miongozo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Udahili, Utahini na Utunuku, Dkt. Marcelina Baitilwake amewaasa wakuu wa vyuo kufuatilia mchakato wa udahili kwa karibu kwa watendaji wao ngazi za chini ili kuhakikisha masharti yanazingatiwa.

Dkt. Baitilwake amesema NACTVET ina shabaha moja tu ya kuhakikisha Mfumo wa Udahili wa Pamoja unafanya kazi kama ulivyokusudiwa, hivyo wahusika wa eneo la Udahili kwenye vyuo hawana budi kuzingatia yawapasayo kufanya ili kufanikisha Udahili kwa kuzingatia miongozo iliyopo.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vyuo Binafsi vya Afya nchini (APHCOT) Dkt. Joel Limbu Maduhu ameishukuru NACTVET kwa kuitisha kikao hicho kwa lengo la kubaini changamoto za udahili na kuzijadili kwa pamoja na wadau wa vyuo vya afya, ili kuzitafutia majawabu sahihi.

Dkt. Maduhu amewataka maafisa udahili na mitihani kwenye vyuo vya afya kupunguza changamoto za udahili kwa kutekeleza maelekezo ya NACTVET. Amewaomba wadau wa APHECOT kuwa na Subira kila zinapojitokeza changamoto za kimfumo wakati wa udahili na kuziwasilisha kwenye ngazi husika ili kupata suluhu ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad