HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 11, 2023

UDSM, SEKTA BINAFSI WAWEKA MIKAKATI KWA WAHITIMU VYUO VIKUU

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Raphael Maganga akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye mazungumzo ya kimkakati baina yao na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhusu namna ya kuwasaidia wahitimu wa vyuo vikuu katika sekta hiyo binafsi. 

Picha ya pamoja baina ya Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na baadhi ya Wadau na Wakuu wa Taasisi za sekta binafsi.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Jacqueline Lohay Woiso akizungumza namna ya vyuo vikuu vitakavyowasaidia wahitimu pindi wanapopata nafasi katika sekta binafsi.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. William Anangisye akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Kongamano baina yao na Wadau wa sekta binafsi, Kongamano lenye lengo la kufanya mazungumzo ya kimkakati ili kuwasaidia ujuzi wahitimu wa vyuo vikuu ili kuleta tija kwenye sekta hiyo na taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kutoka kushoto) akichangia mada kwenye jopo lililoandaliwa kwenye Kongamano hilo.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wadau wa sekta binafsi nchini wameendelea kuweka mipango mikakati ya kuwaandaa vijana wanaohitimu mafunzo ya ngazi ya elimu ya juu ili kuajirika, kuwa wazalishaji wazuri na kuchangia maendeleo ya taifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Kongamano mahsusi baina ya UDSM na wadau wa sekta binafsi, Makamu Mkuu - UDSM, Prof. William Anangisye amesema wamekutana na sekta hiyo ili kujadiliana namna ya kuwasaidia vijana hao wanaohitimu mafunzo yao sanjari na kuwawezesha kufikiria kujiajiri kwa maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla.

“Tumewaita sekta binafsi hususani Maafisa Watendaji wakuu wa sekta hii, lengo ni kufanya nao mazungumzo ya kimkakati ili kushauriana nao na kujifunza kwao kwenye masuala yanayowahusu wahitimu wa vyuo vikuu ili wahitimu hawa waweze kuajirika na kuleta manufaa kwa taifa la Tanzania,” amesema Prof. Anangisye.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Raphael Maganga amesema kupitia mazungumzo hayo kati yao na UDSM, wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuboresha mitaala ya vyuo vikuu na kuweka mitaala ambayo ni rafiki kwa wahitimu wanaoliza vyuoni humo.

Maganga amesema wameshauriana pia namna ya kuwapa ujuzi wahitimu hao ambao wengine wanapata nafasi za ajira katika sekta hiyo binafsi, amesema ni wajibu wa vyuo hivyo na sekta hizo binafsi kuwapatia ujuzi wahitimu hao ikiwemo kuwasaidia kwenye masuala ya nidhamu na uwezo wa mawasiliano.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Jacqueline Lohay Woiso ameshauri wahitimu hao pindi wawapo vyuoni kusaidiwa hususani kupewa ujuzi wa huduma kwa wateja, namna ya kuhudumia vizuri wateja katika sekta hizo, pia kupewa mafunzo ya uwezo wa kuwasiliana na Wakuu wa Taasisi hizo sanjari na Wafanyakazi wenzao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad