HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 11, 2023

NACTVET yatoa matokeo ya waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi

 

Mkurugenzi wa Udahili, Utahini na Utunuku wa Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Dkt. Marcelina Baitilwake akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matokeo ya wanafunzi wanaojiunga na  vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi  kwa mwaka wa masomo 2023/2024,  jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Utahini na Utunuku wa Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Twaha Twaha akizungumza kuhusiana na utaratibu unaotumika kwa wanafunzi kujiunga na vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi , jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
BALAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limesema kuwa limetangaza matokeo ya uchaguzi wa awamu ya kwanza wa program za Afya na sayansi Shirikishi.

Udahili wa wanafunzi wa kozi mbalumbali za afya na sayansi shirikishi kupitia mfumo wa wa udahili wa pamoja (CAS)kwa mwaka wa masomo 2023/2023 kwa kuwa na wanafunzi waliomba 24, 007 kati ya hao waliokamilisha maombi hayo ni wanafunzi 20, 234 huku waliokosa sifa kwenye program hizo ni 2,034

Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo Mkurugenzi wa Udahili , Utahini na Utunuku Dkt.Marcelina Baitilwaake amesema kuwa waombaji 15, 833 wamechaguliwa kujiunga kwenye vyuo 219 vinavyotoa program mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi ambapo kati hao wanawake 8, 248 sawa na asilimia 52 na wanaume 7, 585 sawa na asilimia 48 ambapo waombaji 2, 868 walishaguliwa kwenye vyuo 48 vya serikali na waombaji 12, 965 wamechanguliwa kwenye vyuo vya sekta binafsi.

Amesema waombaji wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kwenye program hiyo ni kutokana na ushindani uliokuwepo kwenye vyuo walivyoomba na kushauriwa kuomba awamu nyingine kwa program na vyuo vyenye nafasi katika dirisha kupitia mfumo wa udahili wa pamoja (CAS) ambao umefunguliwa Julai 11, 2023 hadi Agasti 8, 2023 na matokeo yake yatatolewa Agasti 13, 2023.

Waombaji wote wanaweza kuangalia matokeo yao ya uchaguzi kupitia tovuti ya Baraza.www.nacte.go.tz kwa kubonyeza CAS selection 2023 kwa ajili ya kupata taarifa zaidi

Meneja wa Utahini na Utunuku wa NACTVET Twaha Twaha amesema kuwa wanafunzi 2,034 waliokosa sifa wanaweza kuomba tena kwenye program hiyo kwa kozi nyingine.

Amesema kuwa sifa hizo zinatakiwa kuwa mwanafunzi wa ufaulu masomo manne hivyo kuna kozi zingine zina masomo matatu ambapo walikosa katika sifa za awali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad