HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 1, 2023

Tafiti zaonesha sheria ya manunuzi bado kusaidia wanawake


Na Mwandishi wetu

PAMOJA na Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 kufanyiwa marekebisho ili kuhusisha makundi ya Vijana, Wanawake, Wazee na Watu Wenye Ulemavu kama kundi maalumu bado wanawake wamekuwa hawashiriki kikamilifu katika fursa za zabuni zilizopo kwa mujibu wa sheria.

Mabadiliko hayo pia yalitaka taasisi zinazofanya manunuzi kutenga angalau asilimia 30 ya bajeti yao ya manunuzi kwa ajili ya makundi maalumu, wakiwemo wanawake.

Kauli hiyo imetolewa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Prof. Samwel Wangwe katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu  wa taasisi hiyo, Deodatus Sagamiko kwenye“Sera ya Biashara” (2003) inalenga kuinua ufanisi, kupanua uhusiano katika uzalishaji wa ndani na kujenga sekta ya ushindani wa mauzo ya nje ili kuchochea ukuaji na maendeleo nchini Tanzania. Sera inataja haja ya "kuunga mkono ushirikishwaji wa wanawake katika michakato ya maendeleo ya biashara kupitia upatikanaji wa usawa zaidi wa mali za uzalishaji, hasa ardhi yenye hati miliki, miundombinu, fedha, elimu na ujuzi," alisema Profesa Wangwe akikariri vifungu vinavyowezesha wanawake katika biashara ya zabuni.

Pia, aliongeza kuwa sheria hiyo imetoa maelekezo ya mafunzo na kurekebisha taratibu za uendeshaji ili kuruhusu na kukuza matumizi ya mfumo wa ununuzi wa umma; kushughulikia vikwazo vya kifedha na upatikanaji wa taarifa za ununuzi wa umma ili kunufaisha makundi maalumu.

Alisema Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) iliyoanzishwa mwaka 1994 kama taasisi huru ya utafiti na uchambuzi wa sera, ikiwa na Malengo ya kimsingi ni kuimarisha uwezo katika uchanganuzi wa sera na usimamizi wa maendeleo na kuongeza uelewa wa sera katika serikali, sekta ya umma, mashirika ya kiraia, na jumuiya ya wafadhili na ukuaji wa sekta binafsi, ilifanya utafiti huo kuona hatua zipi za makusudi zinaweza kuchukuliwa kuwawezesha wanawake kutumia fursa zilizopo katika sheria ya manunuzi.

“Ushiriki katika Ununuzi wa Umma umeonekana kuwa na matokeo makubwa katika uchumi wa Nchi endapo utasimamiwa vyema, “ alisema Profeaa Wangwe akirejea tafiti zilizofanyika ambapo Aprili mwaka huu ilifanyika

Akiwasiliana utafiti huo ESRF na wadau wengine kutoka REPOA na WSP mmoja wa watafiti, Mtafiti Mkuu wa mradi  huo kutoka ESRF wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini,  unaofadhiliwa na IDRC ya Canada,Vivian Kazi alisema kuna haja kubwa ya watunga sera kuendesha kampeni na kuweka utekelezaji murua unaogusa sheria hizo kwa manufaa ya hayo makundi maalumu.

Mradi wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika zabuni za umma ulianza mwaka 2021 Disemba kwa miezi 30 (mpaka mwezi wa nane 2024) na unatekelezwa na taasisi tatu, ESRF ikiwa taasisi kiongozi na wengine ni REPOA na WSP.

Aidha mradi huo unafadhiliwa na IDRC (Canada) umeanza utafiti mwaka 2022 hadi robo ya kwanza ya 2023  kwa mikoa ya Dar es salaam na Dodoma uliwasilisha matokeo ya utafiti kwa wadau wa serikali kuu, Dodoma Aprili  23 mwaka huu na kuanzia Mwezi Mei watafiti wa Taasisi ya WSP walianza mafunzo kwa wajasiriamali jijini Dar es salaam na kwa wilaya zote.

Pia mradi umetengeneza Mkakati wa Mawasiliano ili kuongeza uelewa miongoni mwa watunga sera katika ngazi za wizara na sheria, watu binafsi na WOSMEs kuhusu manunuzi ya umma yanayozingatia jinsia.

Aidha ERSF imesema katika warsha hiyo itaendelea kuwa chombo kurahisisha mawasiliano na watunga sera, kuhusiana na matatizo ya makundi yaliyo hatarini ili kuimarisha midahalo ya kuweka sawa mazingira wezeshi kwa makundi maalumu.

Katika utafiti huo Wadau kadhaa walihojiwa ikiwa ni pamoja na makampuni zaidi ya 3,800 kutoka Dar es Salaam na wadau wengine wakuu kutoka Wizara, Idara na Wakala za Serikali (MDAs), wawakilishi kutoka sekta binafsi pamoja na NGOs..

Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Deodatus Sagamiko akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtafiti Mkuu wa mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini, Vivian Kazi wa ESRF akitoa muhtasari wa mradi wakati wa warsha  hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtafiti Mshiriki wa ESRF Prof. Linda Mhando akiwasilisha mada ya mkakati wa mawasiliano wakati wa warsha ya mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini kutoka ESRF, Geroge Temba akiwasilisha malengo ya mradi kwa washiriki wa mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtafiti mshiriki mwandamizi kutoka REPOA, Prof. Paschal Mihyo akitoa maelezo kuhusu awamu ya pili na tatu ya mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtafiti na mratibu wa miradi  kutok INSP Tanzania, Habambi Habambi akiwasilisha mada kuhusu awamu ya pili na tatu ya mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Programu ya uwezeshaji wanawake kiuchumi wa UN WOMEN nchini, Lilian Mwamdanga  (katikati) akichokoza mada kwa washiriki (hawapo pichani) wa mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dr Rose Reuben na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC, Bi. Mwajuma Hamza.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dr. Rose Reuben (kulia) akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani) wa mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mtaalamu wa Programu ya uwezeshaji wanawake kiuchumi wa UN WOMEN nchini, Lilian Mwamdanga  na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC, Bi. Mwajuma Hamza. 
Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC, Bi. Mwajuma Hamza (kushoto)akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtaalamu wa Programu ya uwezeshaji wanawake kiuchumi wa UN WOMEN nchini, Lilian Mwamdanga.
Mshiriki kutoka TUINUANE Group, Hilda Boniphace akitoa maoni wakati wa warsha ya mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mshiriki kutoka MAWENI CLEANERS Group, Bi. Shani Chaul akichangia mawazo wakati wa warsha ya mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini wakati wa warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Washirki wa warsha mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini walioshirki warsha hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Meza kuu katika picha ya pamoja na washiriki wa mradi unaofadhiliwa na IDRC (Canada) unatekelezwa na taasisi tatu, ESRF ikiwa taasisi kiongozi na wengine ni REPOA na WSP wa kuwezesha wanawake wamiliki wa biashara katika ununuzi wa umma nchini wakati wa warsha iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad