HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 1, 2023

NIC Insurance yaweka mkakati wa kutoa elimu ya uelewa bima nchini

Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Karim Meshack akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya NIC kwenye maonesho 47 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko  na Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Karim Meshack akizungumza kuhusiana na mikakati ya kutoa elimu ya bima kwa watanzania kwenye maonesho 47 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

*Yabainisha watumiaji wa Bima ni asilimia 1.86.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.

NIC Insurance imesema kuwa takwimu za watumiaji wa bima ziko chini kwa asilimia 1.86 hivyo NIC kazi yake ni kuelimisha kwa elimu ya uelewa wa Bima ili kufikia asilimia kubwa kuliko ilivyo sasa.

Akizungumza katika Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba)Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano Karim Meshack amesema NIC katika maonesho hayo watatoa elimu ya bima pamoja na faida za bima kutokana tafiti walizo nazo ili kila mtanzania awe na uelewa wa bima.

Amesema kuwa jamii ilikuwa inajua suala la bima ilikuwa ikilenga matajiri tu hali ambayo ilifanya jamii kubwa kutotaka kujua bima hivyo NIC inataka kwa nguvu zote jamii kuachana na hiyo.

Amesema Watanzania wamewapa dhamana NIC katika kuwalinda katika majanga yanayowakuta kutatuliwa na bima.

Meshack amesema Mtanzania anajenga nyumba ya shilingi milioni 100 lakini inaungua kwa moto kwa dakika 10 ambapo akiwa na bima ya kulipia 177000 inamfanya kuondoa hofu kutokana na kupata nyumba nyingine kutokana na bina aliyoikata.

Amesema katika bidhaa za bima watanzania wanaweza kukata bima ya maisha ambapo ikitokea baba au mama walikata bima NIC itatoa bima kwa familia iliyobaki katika kuendesha maisha na kufanya waliofiwa kulia kwa kuondokewa na mtu lakini maisha yao yataendelea kama kawaida.

Aidha amesema bidhaa nyingine ya Bima ni Beam Life na uwekezaji ambapo aliyekata atafapata faida ya asilimia Saba kwa mwaka.
Amesema aliyekata Bima ya Beam Life akifariki NIC itatoa mkono wa pole asilimia 5 ambayo haitoki kwenye fedha aliyoweka.

Amesma NIC kazi yake ni kuangalia changamoto kwa jamii na kwenda kutatua hizo changamoto kwa watu wa chini ikiwemo mama lishe, Waendesha Bodaboda na makundi mengine.

Hata hivyo amesema kuwa wamekwenda mbali kwa kugusa sekta ya kilimo kwa kuwa na bima ya kilimo ambayo inamlinda mkulima kwa ukame na mafuriko ambapo bima hiyo inamuondoa hofu mkulima akilima na mvua isiponyesha gharama zake zitarudishwa na NIC kutokana bima yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad