Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Dkt.Elirehema Doriye akizungumza na waandishi habari kweyye banda la NIC Insurance kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
*Dkt.Doriye aahidi kwenda kasi na Teknolojia ya Kiditali kwenye utoaji wa huduma za bima
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MKURUGENZI Mtendaji wa NIC Insurance Dkt.Elirehema Doriye amesema miaka 60 ya NIC Insurance ni mapinduzi makubwa yamefanyika katika kutoa huduma za bima nchini.
Dkt.Doriye ameyasema hayo kwenye banda la NIC Insurance kwenye maonesho ya Biashara Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Amesema safari ya miaka 60 ilikuwa ya mabonde na milima lakini sasa mapinduzi yamefanyika katika NIC kutumia ubunifu kwenye mapinduzi ya teknolojia kwa kutengeneza mifumo ya Kidijitali ya kuwafikia kiurahisi na kufanya huduma zetu kuingia sokoni na kupokelewa kiurahisi.
Amesema katika mapinduzi ya Teknolojia NIC imeweza kupata Tunzo ya Superbrands Afrika Mashariki ambapo makapuni mengine hayajafikia tunzo hiyo.
"Mafanikio yetu yanatokana na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kufungua mipaka ya uwekezaji na biashara na kufanya NIC Insurance kupita katumia mipaka hiyo iliyofunguliwa na Rais Wetu"amesema Dkt.Doriye.
Amesema kuwa kasi yao haitaishia hapo kwani watanzania wanaitegemea NIC katika kuwafikia kutoa huduma za bima ili waweze kujenga uchumi ambao hata majanga yakitokea NIC kuwashika mkono kutokana na bima zao.
Hata hivyo amesema kuwa miaka 60 hiyo kwao ni sehemu ya deni kwa watanzania katika kuhakikisha wanawafikia katika makundi yote na kuwa NIC Insurance ni kimbilio la huduma bora za bima.
Aidha amesma kuwa NIC Insurance imekwenda mbali hadi kupata cheti cha kimataifa cha ISO kutokana na kutoa huduma bora kwa wateja
Amesema NIC Insurance naendelea kuboresha huduma kwa viwango vya Kimataifa kwa sababu wanauzoefu katika bima wataendelea kuwa bora zaidi.
"Safari ya miaka 60 ilikuwa ya misusuko na changamoto mbalimbali ambazo ndizo zilizofanya kuwa bora katika utoaji wa huduma bora na imetupa hekima ya kuelezea watanzania wanataka nini na wanamuangalia mteja uwezo wa kumhudumia vizuri Ili twende na viwango vya Kimataifa kiwango kisicho pungua asilimia 90,"amesema Dkt. Doriye
Amesema wanaendana na mabadiliko ya uchumi na Teknolojia katika utoaji bidhaa za bima zinazohutajika katika soko.
Aidha aesema bidhaa ambazo wanatengeneza kwenye bima za na bima za Maisha, Beam Life, Kilimo na nyinginezo kutokana na soko linavyokwenda katika mahitaji ya wananchi.
No comments:
Post a Comment