HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 14, 2023

NBAA YAWAKUTANISHA WADAU KUPITIA NA KUJADILI MTAALA WA BODI

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu akizungumza na wadau waliofika kwenye mkutano wa kujadili na kupitia Mtaala mpya wa Masomo ya Bodi uliofanyika katika ukumbi wa NBAA jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo, Peter Lyimo akitoa maelezo kuhusu mtaala mpya wa Masomo ya Bodi kwa wadau waliofika kupitia na kujadili mtaala huo uliofanyika katika ukumbi wa NBAA jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia Temu alipokuwa anafungua mkutano wa wadau waliofika kujadili na kupitia  Mtaala mpya wa Masomo uliofanyika katika ukumbi wa NBAA jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye makundi mbalimbali wakipitia na kujadili mtaala Mpya wa Masomo ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akiendesha mjadala wa kujadili na kupitia mtaala mpya wa Masomo ya NBAA kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali na kufanyika katika ukumbi wa NBAA jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau walioshiriki mkutano wa kujadili na kupitia mtaala mpya wa masomo ya Bodi wakitoa maoni yao kuhusu Mtaala  huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akifunga mkutano wa wadau waliofika kujadili na kupitia mtaala Mpya wa Masomo ya  Bodi uliofanyika katika ukumbi wa NBAA jijini Dar es Salaam.

1 comment:

  1. Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA inawashukuru kwa mara nyingi tena wadau wote walohudhria Kongamano la leo na wale ambao waliokwisha wasilisha maoni yao kuhusu Marejeo ya Mitaala inayoendelea.

    Milango ya NBAA iko wazi kupitia njia mbalimbali kupokea maoni ya kuongeza Ubora wa Utendaji wa NBAA hususan mtihani na mafunzo endelevu (CPD programs).

    ReplyDelete

Post Bottom Ad