HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 14, 2023

MBUNGE NGASSA: WANANCHI MSITETELEKE MPO SALAMA KWENYE MIKONO YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Mbunge Ngassa (kushoto) akitoa maelekezo ya ukarabati wa Zahanati ya Mwamapuli kwa Muuguzi Afya wa zahanati hiyo. 

Wakina mama wakimlaki Mbunge wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora, Nicholaus Ngassa wakati wa ziara yake aliyoifanya jimboni humo mara baada ya vikao vya Bunge la Bajeti kumalizika hivi karibuni, ambayo ilikwenda sanjari na mikutano ya hadhara.

Na Mwandishi Wetu, Igunga
MBUNGE wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora Mhe. Nicholaus Ngassa amewaomba wananchi wa jimbo hilo kutoteteleka kwa kauli mbalimbali za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu, kuhusu maendeleo na kuwahakikishia kuwa chini ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samoa Suluhu Hassan wapo kwenye mikono salama na waendele kupokea miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia Ilani ya Chaka hicho.

Ngassa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wananchi kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara aliyofanya katika Vijiji na Vitongoji vya Kata ya Kinungu.

"Kinungu tumeleta umeme, barabara, maji ya visima ujenzi wa miundombinu ya madarasa kwa shule zote za sekondari na msingi na sasa mjiandae kupokea maji ya Ziwa Victoria kupitia mradi unaotekelezwa kwa thamani ya Sh. Bilioni 20 kutoka kwenye tenki linalojengwa Mlima wa Bulenya.

Watoto wanasoma elimu bure bila malipo,tumeongeza upatikanaji wa madawa na vifaa tiba kwenye vituo vya afya na zahanati za vijijini, haya ndio maendeleo tuliyoahidi mwaka 2020 kwenye kampeni na tunaendelea kutekeleza, " alisema Ngassa.

Ngassa alisema hayo yote yanatekelezwa chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye anatoa fedha nyingi nchi mzima kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

" Binafsi nichukue nafasi ya kipekee kumshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kazi hii kubwa anayoifanya kwenye jimbo letu, mkoa wetu na Taifa kwa ujumla nawaomba ndugu zangu kwa iman zetu tuendelee kumuombea kwa Mungu ampe afya na maisha marefu," alisema Ngassa.

Katika mikutano hiyo Mbunge Ngassa alipata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali na zile zilizokuwa ndani ya uwezo wake alizitafutia ufumbuzi wa papo kwa papo kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga na zile zilizokuwa nje ya uwezo wake alisema ataziwasilisha kwa wahusika


Wananchi wa Kitongoji cha Migunga Kata ya Igunga wakimpokea kwa shangwe Mbunge wao kipenzi Nicholaus Ngassa wakati wa ziara yake jimboni humo.
Mbunge Ngassa akiwa na wanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya Msingi Mwamapuli Kata ya Kinungu, aliowavalisha sare ikiwa ni utekelezaji wa programu ya kugawa sare kwa wanafunzi wa darasa hilo jimboni humo.
Wananchi wa Kitongoji cha Mwanunili Kijiji cha Mwamapuli Kata ya Kinungu wakimsikiliza Mbunge wao Ngassa alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad