HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 14, 2023

DP world kutoa asilimia 35 kwa wazawa

 


MWENYEKITI wa Kamati ya Majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, juu ya uwekezaji bandarini, Hamza Johar, Amesema DP World kabla hajaanza kazi hapa nchini itasajili Kampuni ya kitanzania na asilimia 35 za hisa atatoa kwa wazawa.

Amesema, hakuna mfanyakazi yeyote atakayepoteza ajiira pale bandarini

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kufafanua juu ya mkataba huo Johar amesema, kumekuwa na maswali katika baadhi ya vipengele ikiwemo namna wazawa watakavyoshiriki kwenye uwekezaji huo kabla mkataba haujaingiwa na namna DP World itakayosaidia nchi katika kupata utaalamu kuhusu uendeshaji Bandari Kisasa.

Amesema, katika Ibara ya 13 ya mkataba wamekubaliana kuwa ni lazima DP World iwaajiri wafanyakazi atakaowakuta na itoe kipaumbele kwa kampuni za ndani na kusaidia kujenga vyuo vya mafunzo kama DMW na NIT

"Awali alikataa tukasema kama hawataki basi, tulifanya hivi ilikuwa lazima tumtishe lakini baadae alikubali," amesema Johar na kuongeza kuwa mkataba huo hauna tobo wala dosari yoyote na yuko tayari kukaa popote kuutolea ufafanuzi.

Ameongeza kuwa, katika mkataba wa makubaliano, kuna vipengele vinavyoelekeza DP World kusitishiwa mkataba endapo shughuli zake hazitaendeshwa kwa ufanisi au kukiuka mkataba.

Johar amefafanua kuwa, bandari haujauzwa bali inakodishwa kwa DP World kwa muda ambao utawekwa katika mikataba ya utekelezaji itakayoingiwa hivi karibuni ambapo yeye DP World atapewa asilimia nane ya sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam, na si Bandari nzima kama inavyodaiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad