HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 21, 2023

DC TEMEKE ARIDHISHWA NA UJENZI SOKO JIPYA MBAGALA ZAKHEM , ATOA SIKU 25 MKANDARASI KUKABIDHI SOKO HILO KWA MANISPAA YA TEMEKE

 

DC wa Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi  akielezea jambo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa soko jipya la Mbagala Zakhem  leo Agosti 21 2023 Dar es  Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi ambaye ameshika kipaza  sauti akizungumza na baadhi  ya wafanya biashara wakati alipofanya ziara  leo Agosti 21 ,2023 kwenye soko jipya Mbagala Kibonde Maji 'Zakhem '  Dar es Salaam
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya akifafa jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi  na aliyesimama  wa kwanza  kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Mtinika


Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
MKUU wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Mobhare Matinyi leo Agosti 21 ameridhishwa na hali ya ujenzi wa soko jipya na la Kisasa lililopo Mbagala Kibonde Maji (Zakhem) huku akimtaka mkandarasi wa soko hilo kulikabidhi kwa Manispaa ya Temeke ifikapo Agosti 15 ,2023

Awali ya yote nachukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha Bil.2.843 ambazo zimejenga soko hili jipa na la kisasa ndani ya Manispaa ya Temeke, nachukua fursa hii kusema kuwa baada ya mkandarasi kukabidhi soko hili kazi inayobaki ni kwa Mkurugenzi Elihuruma Mabelya wa Manispaa ya Temeke, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Mtinika pamoja na Katibu wa wafanya biashara katika soko hili waketi pamoja na kupanga namna wafanyabiashara watakavyo pangwa ndani ya soko huku kipaumbele kikiwa ni kwa wale wafanyabiashara ambao walikuwepo awali wakati wa lile soko duni.

"Viongozi mtatakiwa kusimamia mgawanyiko wa vizimba vya biashara kulingana na ukubwa wa biashara " amesema Matinyi.

Pia jumla ya mamalishe 20 waliokuwepo awali watapewa kipaumbele ndani ya soko hilo, amesema Mheshimiwa Matinyi.

Amesema kuwa ujenzi wa soko hilo umechukua muda wa mwaka mmoja kikamilifu ambapo awali kulikua na soko duni ambapo hivi sasa kuna vizimba 160 hukumiundo mbinu ikiwa ni rafiki na kufikika kwa urahisi kwa ujumla.

Katika soko hili kutakua na ofisi za Manispaa ambao watasimamaia masuala.ya msingi ndani ya soko pia kutakuwa na kitengo cha Tehama ambacho kitafunga mitambo maalumu ili kufuatilia nyendo zote za wafanyabiashara na utendaji wao kazi ndani ya soko, huku ametoa onyo kali kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa wafanyabiashara ambao watafanya uhuni endapo watapangishwa kwa fedha ndogo ya serikali halafu na wao wapangishe wafanyabiashara wengine.

Wakati huohuo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya amesema kuwa wamejipanga kuwaondoa wafanyabiashara ambao huzagaa hovyo pembezoni mwa barabara kwa kuwa wanakwenda kinyume na sheria huku akisisitiza kwa kusema kuwa Manispaa hiyo wamejipanga na wataanzisha kampeni ya kuwaondoa pamoja kuiweka Temeke safi kwa ujumla.

"Tumetenga kiasi cha Bil.1 ambazo zitafanya ukarabati wa masoko ndani ya Manispaa ya Temeke huku amesisitiza kwa kusema kuwa wafanyabiashara wanaokaa pembezoni mwa barabara si wa Dar es Salaam pekee bali nchi nzima wanakua sawa na uchafu kutokana na kuzagaa hovyo hivyo wamejipanga kuanzisha kampeni ya usafi ndani ya Manispaa ya Temeke itakayoanza hivi karibuni na kutekelezwa usiku na mchana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad