Mratibu Mradi huo na Mratibu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora, Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Lusekelo Kasongwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa kodi leo Julai 21, 2023. Kulia ni Kaimu RASI wa Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Mary Rutenge Kaimu RASI wa Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Mary Rutenge akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa kodi leo Julai 21, 2023. Kulia ni Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu Mzumbe- Morogoro, Dkt. Joseph Kiria.
KATIKA kutekeleza Mradi wa Kodi za Majengo (Property Tax) Unaotekelezwa katika nchi tatu za Afrika, Chuo Kikuu Mzumbe wakishirikiana na Chuo cha Norwegian Institute of International Affairs (NUPI) wanabadilishana uzoefu juu ya mradi huo na wadau wa kisekta.
Mradi huo unatekelezwa katika Nchi tatu za Afrika ambazo ni Tanzania, Mali na Liberia na Unafadhiliwa na Baraza la Tafiti la Norway (Research Council of Norway).
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Julai 21, 2023 wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Akimwakilishwa RASI wa Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Mary Rutenge amesema kuwa ni wakati muafaka wa kufanya mageuzi ya kodi za mali ili kuhakikisha kuwa wanachukua hatua za makusudi kuboresha utendaji na ufanisi wa mifumo inayohusiana na ukusanyaji kodi hizo.
Amesema kuwa Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekabiliwa na changamoto za kukusanya mapato kwa kodi ya mjengo kwa ufanisi na changamoto hizo zimeathiri uwezo wa kutoa huduma bora za umma na kugharamia miradi muhimu ya maendeleo.
Dkt. Rutenge amesema kuwa lengo kuu katika mkutano huu ni kujadili njia bora za kuongeza ukusanyaji wa kodi ya majengo kwa njia endelevu na yenye haki.
Pia ametambua umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, taasisi za elimu, na wadau wengine wa kodi katika kufanikisha mageuzi katika kodi za Mali.
“Tunaamini kuwa mkutano huu utatoa fursa ya kujenga mahusiano bora na kushirikiana katika kutafuta suluhisho la pamoja.
Tunaishukuru Serikali ya Norway kwa kutoa msaada na kuunga mkono juhudi za kuendeleza sekta ya kodi na kukuza mapato ya serikali kupitia kodi za mali.” Amesema Dkt. Rutenge
Akizungumzia malengo ya mkutano huo, Mratibu Mradi huo na Mratibu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora, Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Lusekelo Kasongwa amesema kuwa wanabadilishana uzoefu kwenye masuala ya kodi za majengo (Property Tax) baada ya Tanzania kutumia mfumo wa ukusanyaji kodi hiyo kwa kutumia Ankara za umeme.
Amesema kuwa mkutano huo wanataka kujua changamoto zilizopo, fursa pamoja na kuangalia nini kifafanyike kuboresha mfumo huo.
Kwa Upande wa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu Mzumbe- Morogoro, Dkt. Joseph Kiria amesema kuwa Kuna miradi miwili inayotekelezwa sambamba inayohusiana na usimamizi wa kodi kwa nchi za Afrika.
Amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zilifanikiwa katika ukusanyaji wa kodi hiyo hivyo nchi za Afrika zinachakujifunza kuhusiana na masuala ya ukusanyaji wa kodi.
Amesema kuwa nchi za Mali na Liberi zinashiriki katika mradi huo lakini zinachangamoto ya vita lakini wanatakiwa kushiriki kikamilifu ili waweze kuiga mazuri katika ukusanyaji wa kodi kwa Tanzania.
Wadau walioshiriki katika mkutano huo ni kutoka katika sekta ya umeme, wamiliki wanyumba, sekta za umma, binafsi, Watathmini majengo, wawakilishi wa Serikali za mitaa pamoja na wanazuoni.
Baadhi ya wadau wa Kosi wakichangia maada katika Mkutano wa kubadilishana uzoefu juu ya Mradi wa Kodi za Majengo (Property Tax) iliyofanyika chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo Julai 21, 2023.
Baadhi ya wadau wa Kodi wakiwa katika amkutano ulioandaliwa na chuo Kikuu Mzumbe.
No comments:
Post a Comment